GET /api/v0.1/hansard/entries/723163/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 723163,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/723163/?format=api",
    "text_counter": 265,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Kipyegon",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 1453,
        "legal_name": "Johana Ngeno Kipyegon",
        "slug": "johana-ngeno-kipyegon"
    },
    "content": "liliangamizwa, basi inawezekana kumaliza janga hili. Rais Kibaki alimkubalia mwendazake Waziri Michuki kumaliza kundi la Mungiki lililokuwa likiwahangaisha wakazi katika eneo la Kati mwa Kenya. Michuki hakujali kama Wakikuyu watamlaani. Janga la wizi wa mifugo linafanyika katika eneo la Bonde la Ufa, sehemu ambako Gen. Nkaissery na Naibu wa Rais wametoka. Ni lazima wasimamishe vifo vya watu. Gen. Nkaissery afuate nyayo za Michuki. Naibu wa Rais yuko Serikalini na ni lazima asimamishe vifo vya watu. Serikali tu ndiyo inaweza kumaliza wizi wa mifugo kwa sababu iko na ripoti kuwahusu watu ambao wanahusika na vitendo hivyo. Hatuwezi kumwambia Mhe. Ng’ongo, Kamama na Cheptumo wawakamate wale wanaohusika. Lakini inafaa Serikali itekeleze jukumu la kumaliza janga hili. Hatutashinda tukiwaambia watu wajisajili kama wapiga kura ilhali kuna wale ambao wanakufa. Je, wale wanaouwawa watapiga kura? Tunaiambia Serikali ichukue jukumu hili. Hata katika Eneo Bunge langu, kuna mtu yuko hospitalini ambaye amepigwa risasi sijui ngapi. Juzi tulizika kijana aliyeuawa kwa kukatakatwa mara kumi. Watu kutoka jamii za Maasai na Kipsigis wanakufa na hakuna mtu anayejali. Nkaissery na Naibu Rais hawajakanyanga kule. Hawa watu watakufa mpaka lini? Lazima tuiambie Serikali iamka imalize ukosefu wa usalama nchini. Kama hawatafanya hivyo, uchaguzi utakuwa wa bure. Kama watu wetu wamekufa, nani atapiga kura na watapigia nani kura? Watapiga kura ya nini kama Serikali yenyewe haiwezi kuamka na kumaliza tatizo la ukosefu wa usalama. Ndugu zangu, naiambia Serikali kwamba wakati umefika wa kumaliza ukosefu wa usalama. Tunataka kuishi kwa amani na mipaka yetu iwe na amani. Naomba Serikali ichukue jukumu lake."
}