GET /api/v0.1/hansard/entries/723168/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 723168,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/723168/?format=api",
    "text_counter": 270,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Bady",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 1612,
        "legal_name": "Bady Twalib Bady",
        "slug": "bady-twalib-bady"
    },
    "content": "Asante, Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia fursa pia kuchangia Hoja hii. Nampongeza Mbunge mwenzangu, Mhe. Cheptumo, kwa kuileta Hoja hii. Serikali ina jukumu kubwa sana kuona namna gani itakavyodhibiti hali ya amani katika sehemu ya Baringo. Isiwe Baringo peke yake bali iwe ni Kenya nzima. Ningepenga kutoa mfano wa vile Mhe. Shebesh alivyosema kuhusu Mungiki . Serikali ilipoamua kuwa inataka kuiondoa, Mungiki iliweza kuondoka. Ni muhimu kwa Serikali ya Mhe. Uhuru Kenyatta na Mhe. William Ruto kusimama kidete pamoja na Jenerali Nkaissery kuona kuwa maafa haya yanayoendelea kiholela yametatuliwa. Wakati wa nyuma, tuliona watu wa Sabaot wakiahidiwa na Serikali watatolewa na hii leo Sabaot imetulia. Ni kwa nini leo, hali ilivyo Baringo?"
}