GET /api/v0.1/hansard/entries/724407/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 724407,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/724407/?format=api",
    "text_counter": 105,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Chidzuga",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 751,
        "legal_name": "Zainab Kalekye Chidzuga",
        "slug": "zainab-kalekye-chidzuga"
    },
    "content": "Shukrani Mhe. Spika. Nachukua fursa hi kwanza kumpongeza Rais wetu wa Jamhuri ya Kenya kwa kuona umuhimu wa kumteua mama kuwa Mwenyekiti wa Tume inayosimamia ugavi wa rasilimali. Kusema ukweli, hii Kamati ambayo ilimhoji huyu mama waliona ni mama ambaye ana utaalamu na elimu ambayo kati ya wengi na waume walikuwa, akaibuka kwamba ndiye mjuzi kushinda wale wengine wote – kielimu na kiutaalamu. Ameweza kutumikia Serikali na jamii ndani na nje ya nchi. Ni mama ambaye katika wadhifa wake, atasimamia rasilimali zetu na kuona ugavi wa haki na wa usawa katika nchi nzima. Tukiangalia nchi nzima, pia nitoe wito kwake aangalie maeneo ambayo yameathirika zaidi. Yameathirika kimaumbile na sio kwa sababu ya watu kupenda bali ndivyo yalivyoumbwa. Kwa mfano, kuna maeneo ya Turkana, Isiolo, Kaskazini Mashariki, sehemu za Pwani ikimewo Kwale. Waangalie vile tutapata mgao wetu kwa wakati unaofaa na utumike kwa njia inayofaa. Katika hali ya akina mama, mara nyingi ndio wanaojua jinsi ya kugawa. Natoa wito kwake asiwe kiongozi wa ndani ya ofisi, atoke atembee nyanjani, atushirikishe sisi viongozi wa mashinani ili tutembee na yeye, aweze kujionea mwenyewe ili akitoa uamuzi, awe anatoa uamuzi wa kisawasawa, ikiwa ni kitu ambacho yeye mwenyewe amejionea kwa macho. Pia nitoe witu kwa Wabunge wenzangu kwamba hii nafasi kwa huyu mama ni nafasi ambayo imekuja kwa wakati unaofaa, hasa mkiangalia ile hali tulio nayo ya njaa katika nchi yetu ya Kenya. Saa hii kuna shida nyingi za njaa. Kuna shida kubwa ya maji. Kuna shida kubwa upande wa usalama. Hayo yote yameletwa kwa sababu hakujakuwa na usawa wa ugavi wa rasilimali. Lakini tutakapompa nafasi Daktari, nina imani tutakuwa tumejijenga kwa kumtukuza mama ambaye ana ujuzi wa kugawa. Kawaida yetu akina mama, hata ukimwachia shilingi hamsini juu ya meza, utakwenda uendako halafu ukirudi, utapata ugali juu ya meza na watoto watakuwa sawa. Kwa hivyo, hii nafasi mkimpatia daktari, itabidi tuwe na imani kwamba ugavi utakuwa wa usawa bila upendeleo. Shukrani kwa Rais wetu kwa kuweza kuona mbali na kumpatia mama hii nafasi, na sisi Wabunge tunaunga mkono kwa pamoja. Shukrani, Bwana Spika."
}