GET /api/v0.1/hansard/entries/725207/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 725207,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/725207/?format=api",
"text_counter": 94,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Gichigi",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1909,
"legal_name": "Samuel Kamunye Gichigi",
"slug": "samuel-kamunye-gichigi"
},
"content": "Asante sana, Mhe. Naibu Spika. Naunga mkono Mswada huu na kumpongeza Mhe. Abdinoor kwa kuleta pendekezo la kisheria, ambalo likipitishwa litasaidia nchi hii. Sekta ya mifugo ni muhimu sana katika nchi hii kwa sababu hata wale ambao si wafugaji wana mifugo. Katika eneo la Kipipiri na Nyandarua Kaunti kwa jumla, karibu kila boma lina ng’ombe, kondoo na mbuzi. Ijapokuwa wakulima hao wanalima mimea mbalimbali, kutokuwa na mifugo inatokana na umaskini, ama waliuza mifugo wao kulipa karo. Isisemekane kuwa mifugo ni muhimu tu kwa maeneo kavu kwa sababu hata kwenye maeneo yetu, tuna mifugo. Ninaunga mkono kuundwa kwa halmashauri ambayo itasimamia mambo ya mifugo, haswa kutafuta soko na kuangalia magonjwa ya mifugo. Halmashauri hiyo pia inafaa kuhakikisha kwamba mifugo ambao wanawekwa nchini wanatoka katika sehemu mbalimbali. Pendekezo katika Mswada huu ni kuwa wanachama wa halmashauri hiyo watakuwa ofisini kwa miaka minne. Nina pendekezo tofauti. Kwa sababu Katiba imempa Rais kipindi cha miaka mitano, halmashauri za Serikali pia ziweze kuongozwa na wakuu wao kwa miaka mitano. Kumpa kiongozi wa halmashauri miaka mitatu haifai kwa sababu atajua kazi mwaka wa kwanza na mwaka wa pili, atajipanga jinsi atapigania ili aongezewe kipindi cha pili, na huenda asifanye kazi nzuri. Ningependa kupendekeza kuwa sheria zote za halmashauri ziwape wakuu wote kipindi cha miaka mitano ili wafanye kazi nzuri. Halmashauri ikiamua kuwapatia kipindi kingine cha miaka mitano, itakuwa imejua iwapo wamefanya kazi au la. Ningependa kupendekeza pia kuwa halmashauri hii iunganishwe na mambo yanayohusiana na maji. Wakati mwingi, mifugo wetu wanakufa kwa sababu ya ukosefu wa maji. Tukitenganisha mambo ya ufugaji na uenezaji wa huduma ya maji kwa sehemu ambazo zinaathiriwa na ukosefu wa mvua, huenda tusifanikiwe. Bajeti inayopewa sekta ya ufugaji ni The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}