GET /api/v0.1/hansard/entries/725233/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 725233,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/725233/?format=api",
    "text_counter": 120,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Leshoomo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 379,
        "legal_name": "Maison Leshoomo",
        "slug": "maison-leshoomo"
    },
    "content": "Sheria imewekwa kwa kila kitu kinachotengenezwa katika Kenya yetu. Kuna bodi ya sukari, bodi ya kahawa, bodi ya majani na bodi ya kila kitu. Tunaomba tuipitishe hii sheria kwa sababu itasaidia wafugaji wote katika Kenya nzima. Tumetembea na tukaona vile wafugaji wanachunga wanyama wao na vile sheria imewekwa. Tukipitisha hii sheria, itawasaidia wafugaji na wanyama wao. Sheria hii itatusaidia hasa katika wakati wa ukame kama huu. Mwenzangu amesema hajui mahali Kshs450 milioni zimeenda na hiyo pesa inaendelea kununua wanyama katika kila pembe ya Kenya ambayo imeathiriwa na ukame. Ningeomba pesa ipitishwe ili isaidie pande za wanyama yetu. Wafugaji wanaumia sana katika uchungaji wao. Ndio maana kila mtu anasema wafugaji wamehama, wamepeleka ng’ombe na mbuzi zao kwa mashamba ya watu. Wameenda kulisha mifugo yao huko. Wametoka upande huu wanaenda tena upande mwingine. Nafikiri sheria hii ya kulinda wanyama ikipitishwa, itasaidia kila mtu. Pia tunaomba ile idara inasimamia wanyama iangalie ni njia gani itaweza kusaidia kwa sababu pesa nyingi sana zinaitishwa, hata kwa mashirika yasiyo ya Kiserikali kuhusu wanyama wetu, na hazisaidii. Utakuta tu zinaitishwa na haziwezi kusaidia. Tukipata bodi, tunaomba iangalie mambo ya maji zaidi katika pande za wafugaji kwa sababu hiyo ndiyo shida nyingine mbaya zaidi wakati wa ukame. Pia mambo ya ugonjwa, vile wenzangu wamesema. Magonjwa mengi sana hudhuru wanyama."
}