GET /api/v0.1/hansard/entries/725333/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 725333,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/725333/?format=api",
"text_counter": 24,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Tunaongea juu ya kifo cha mwenzetu, sio kicheko. Tulikuwa tunamfurahia. Alikuwa Kiranja wetu. Alikuwa anajulikana sana akisimama kutoa hoja ya nidhamu; hata kama Spika hakutaka kumpa nafasi, ilimbidi ampe nafasi kwa sababu ya sauti na ufasaha alioutumia kwa kutoa hoja zake. Marehemu Sen. Boy Juma Boy alikirithi kiti cha babake, Marehemu Mzee Juma Boy, ambaye alijulikana sana nchini Kenya kama Kiongozi wa wafanyi kazi. Alitembea Kenya mzima kutetea wafanyi kazi katika viwanda vya miwa, karatasi na kwingine. Marehemu Sen. Boy Juma Boy alipokuwa hapa Bungeni alikuwa Mtetezi wa wanyonge kila wakati. Hakuwa mtu wa kusema maneno mengi lakini yale aliyoyasema kwa uchache yalikuwa ya kujenga nchi yetu, kuwatetea watu na kuleta haki na usawa kwa wananchi wa Kenya. Kama kiongozi wa upande wangu katika Seneti hii, naweza kusema kwa furaha ya kwamba marehemu Sen. Boy Juma Boy alikuwa mwadilifu, aliwajibika vilivyo na alikuwa Seneta mwaminifu kwa chama chake, mrengo wetu na Seneti kama vile ndugu yake amesema. Alitenda kazi kwa ufasaha na ushujaa kwa kila kamati aliyoteuliwa kutumikia. Nakumbuka wakati tulimpa nafasi kuketi katika kamati iliyokuwa inachunguza mienendo ya Naibu Gavana wa Machakos, akija kuniuliza na kunieleza vile mambo yalikuwa yanakwenda na msimamo tuliyokusudia kuchukua. Hakuwa mtu wa kujifanyia mwenyewe mambo yanayohusu Seneti hasa mrengo wetu. Mara nyingi alikuwa anakuja kuniuliza, “ Boss, hapa kura tunapiga namna gani?” Ukimwambia msimamo wa mrengo wetu ni huu anasema, “mimi nilikuwa na maoni tofauti, boss, lakini vile wewe umesema, basi sisi tutapiga kura hivyo.” Hiyo ndiyo maana ya demokrasia ya Bunge. Kuna mambo mengi ambayo unaweza kuja Bunge ukiwa na msimamo wako mkali; msimamo ambao pengine una faida kwako kibinafsi lakini lazima ufuate yale mrengo wako na chama chako kimesema.Marehemu Sen. Boy Juma Boy alikuwa mwadilifu kwa mambo hayo. Aliwajibika vilivyo. Sisi sote tulimheshimu, tulimpenda na kumfurahia. Bw. Naibu Spika, tukiwa Vanga, wewe pia ulijionea ya kwamba marehemu Sen. Boy Juma Boy hakubahatisha mrengo wa siasa aliyokuwa. Watu wake walisema kinaga ubaga ya kwamba walifurahia,walikupenda kule alikuwa na watabaki kule alikokuwa. Hayo ndiyo mienendo ya kiongozi ambaye analinda na kuongoza watu wake vilivyo. Nakumbuka wakati wa uchaguzi uliopita, nilikuwa nimeteuliwa na mrengo wetu kwenda kampeni katika kaunti za mkoa wa Pwani. Tulienda kutoka kituo hadi kituo, eneo bunge hadi eneo bunge na marehemu Sen. Boy Juma Boy; popote tulipoenda, watu walimfuhia, The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate"
}