GET /api/v0.1/hansard/entries/725335/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 725335,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/725335/?format=api",
    "text_counter": 26,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "walimjua, walimshangilia na walimahidi ya kwamba angechaguliwa kama Seneta wa Kwale. Alikuwa anabishana na ndugu yetu, Bw. Mwakwere ambaye alikuwa waziri na alikuwa na hela kumliko. Bw. Mwakwere alikuwa na name recognition wakati huo kwa sababu marehemu Sen. Boy Juma Boy alikuwa nje ya Bunge kwa karibu miaka kumi na mitano. Lakini kwa sababu aliyoifanya marehemu babake na yeye pia alipokuwa Bungeni, wananchi wa Kwale walimtunukia nafasi na heshima ya kuwa Seneta wa kwanza wa Kwale katika muhula huu wa pili wa Bunge hili la Seneti. Bw. Naibu Spika, nikimalizia ili wenzangu pia wachangie, ningekuwa mwandashi Shaaban bin Robert aliyeandika kitabu kinachoitwa, Wasifu wa Sid bin Saad ; alisema, “Sidi ni mwana mrembo aliyeumbwa akaumbika.” Boy Juma Boy alikuwa mtu aliyeumbwa akaumbika. Endapo angetembea kwa hatua zake, ungetambua kuwa ni mtu wa heshima. Shaaban Robert alisema kuwa sura ya Sidi ni kama almasi. Boy Juma Boy pia alikuwa mtu wa kupendeza kweli kweli. Shaaban Robert pia alisema kuwa Sidi alipoongea, sauti yake ilitoka kama kinanda. Boy Juma Boy pia alipoongea hapa, hata wale wenye tabia mbovu ya kupigia wenzao kelele katika Bunge walinyamaza na kumsikiliza. Tumempoteza Juma Boy Juma kwa wakati ambao tunaelekea kwenye uchaguzi. Sisi kama mrengo wa the National Super Alliance (NASA) tulikuwa tunamtegemea Boy Juma Boy kwa Kiswahili chache cha machachari na ufasaha wake kama mmoja wetu ambaye tungetembea naye Kenya mzima kueleza Wakenya kwa nini tunahitaji mabadiliko na kwa nini NASA ndio jawabu ya shida za Kenya. Mungu alimpenda kutuliko na ndio sababu alimwita. Jumatano iliyopita, tulikuwa kwa mkutano na tukaambiwa kuwa Boy Juma Boy anaugua na amelazwa katika Hospitali ya Aga Khan. Tuliwatuma Sen. Orengo na Sen. Muthama huko ili kuona kulikuwa na shida gani. Waliporudi, walituambia kuwa alikuwa na shida lakini alikuwa ametolewa chumba cha wagonjwa mahututi na sasa alikuwa amepelekwa katika wadi. Walituambia kuwa alikuwa anaongea, anacheka na amefurahi na waliona hakuna shida. Bw. Naibu Spika, tulipigwa na bumbuazi siku ya Jumapili tuliposikia ya kwamba mwenzetu hayuko tena. Tunaomba Mola amweke mahali pema peponi. Tunaomba wale ambao walimjua kama sisi sote hapa tuige mfano wake wa utetezi bila mapendeleo, kuzungumza manemo bila kuogopa na kupenda nchi yetu vile inatakikana kwa Wakenya wenye nia njema. Asante sana."
}