GET /api/v0.1/hansard/entries/725349/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 725349,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/725349/?format=api",
    "text_counter": 40,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. (Dr.) Machage",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 179,
        "legal_name": "Wilfred Gisuka Machage",
        "slug": "wilfred-machage"
    },
    "content": "Asante Bw. Naibu Spika. Natoa rambi rambi zangu kwa jamii na marafiki wakiwemo wanasiasa wote kwa sababu ya marehemu Boy Juma Boy aliye tuacha hivi juzi. Kwa masikitiko makubwa ningekuwa wakuandika tenzi ya wasifu wa maisha yake, kila mtu angeota machozi kwa sababu alikuwa rafiki wa kila mtu na mcheshi. Sidhani kwamba kuna yeyote hapa ambaye hangependa kuhudhuria mazishi ya marehemu kwa sababu kila Seneta alikuwa rafiiki yake. Alikuwa akiketi hapa karibu nami na siku zote tulikuwa tukitaniana. Yeye ameshauandika ukurasa wake kwa kitabu kikuu. TumepotezaWabunge watatu tangu kuanzishwa kwa hii Seneti kwa mda huo mfupi. Inafaa tukumbuke kwamba sisi sote hapa tuna maisha mafupi na kwamba tutaishia kwa makaburi tu ila siku yetu ya kiamani Mungu pekee anayejua. Ni kudra ya Mungu kwamba uishi kwa siku hizo ambazo amekupa. Nina hakika watu wa Kwale wamempoteza kiongozi mzuri. Hivyo ndivyo Mungu alivyo taka na hatuna budi sisi kuwaombea jamii yake iliyobaki waingiwe na furaha na kusahau kabisa majonzi kwa sababu hivyo ndivyo ilivyo andikwa na hivyo ndivyo ilivyo kwa binadamu. Asante."
}