GET /api/v0.1/hansard/entries/725386/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 725386,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/725386/?format=api",
"text_counter": 77,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kisasa",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13124,
"legal_name": "Mshenga Mvita Kisasa",
"slug": "mshenga-mvita-kisasa"
},
"content": "Asante Bw. Naibu Spika kwa kunipa fursa hii. Marehemu Boy Juma Boy alikuwa akiniita “Sister Du”. Tukiwa hapa Seneti, kisima chetu ni kimoja kwa sababu ni wakati wa kiangazi. Kama ulivyo jionea jana, Sen. Boy Juma Boy alikuwa maji mafuu na mvuvi kafu. Ya malishoni haya letwi mjini. Lakini tungeyaleta hapa leo pasinge kalika. Tuna roho ya simanzi kuomboloze kaka yangu “Brother Du” Boy Juma Boy kwa huzuni. Bahati huwa ina tuangaza lakini huwa haitupi ahadi. Ingekuwa ina fanya hivyo tunge kuwa naye Boy Juma Boy. Tunafaa tujue kuishi vyema kama hapa Seneti. Kijiti kimoja hakijengi nyumba. Jana niliskia vizuri nilivyo ona wenzangu katika Seneti wakija kuomboleza na familia ya Boy Juma Boy. Bwana Naibu Spika, linalo mpata peku na ungo pia litampata pia. Sote tunafaa tuishi vyema. Kifo hakina simanzi, huruma ama mazoea. Kinapo mpata mtoto mdogo huwa tuna sema heri ingekuwa mzee. Akiwa baru baru tuna sema heri angekuwa mtoto mdogo. Akiwa mzee tunasema heri ingekuwa mtu baru baru. Naomba Mwenyezi Mungu aiweke pema peponi roho yake kaka yangu. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate"
}