GET /api/v0.1/hansard/entries/725396/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 725396,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/725396/?format=api",
    "text_counter": 87,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Wangari",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13123,
        "legal_name": "Martha Wangari",
        "slug": "martha-wangari"
    },
    "content": "Asante Bw. Naibu Spika. Naungana na wenzangu kutuma rambi rambi zangu kwa mwenda zake na familia yake Boy Juma Boy na watu wa Kwale. Vile vile nina kushukuru wewe, Bw. Naibu Spika, kwa kuongoza wale walioweza kufika kule Kwale. Kama kifo kingekuwa na rufaa, nina fikiri wale mawakili walioko kwenye Seneti hii wange wasilisha hiyo kesi mara moja. Kama tungepewa wakati wa kusema vile tungetaka, tungekata rufaa. Niliulizwa kuhusu ungonjwa wa mwendazake Boy Juma Boy na Sen. Madzayo siku ya Ijumaa na ni kamuarifu kwamba nita muona jana nikirudi Nairobi. Sikujuwa haingewezekana. Kama ningejua ningerudi hiyo Ijumaa niweze kumuona kabla atuache. Bw. Naibu Spika wa Muda nikikumbuka Sen. Boy Juma Boy, nina kumbuka ufasha wake wa lugha. Nilimjua kwa muda mfupi lakini alinipa ule ukakamavu wa kuweza kutumia lugha ya Kiswahili hapa Bungeni. Hata yale matumizi ya mbinu za lugha, nafikiri hakuna mtu ambaye aliweza kuitumia kuliko hayati Boy Juma Boy. Mambo yakutumia sadfa, methali na utohozi, sidhani kama kuna mtu ambaye angefunza Sen. Boy Juma Boy. Kila siku tutamtamani kwa hili Jumba na kuomba Mungu aweze kuirehemu roho yake na, vile vile, aweze kufariji familia yake ambayo imeachwa. Nina tumaini kwamba yale maadili aliyo yafunza watu; kama mimi alinifunza kuishi nje ya Bunge. Alinieleza kwamba Sen. Wangari ujue ya kwamba siku moja unaweza kuwa nje ya Bunge, kwa hivyo inafaa uishi maisha yakawaida na kutojigamba. Alikuwa anatumia simu ya “MulikaMwizi”, na ungemuuliza anangekujibu: “Makubwa ni ya nini?’ Akija hapa Bungeni, hakuwa na gari kubwa na ninafikiri alitunfunza mengi na Mungu ailaze rohoyake mahali pema peponi. Asante."
}