GET /api/v0.1/hansard/entries/725399/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 725399,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/725399/?format=api",
    "text_counter": 90,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "ya mwenda zake, jamaa na marafiki wake katika Kaunti ya Kwale kwa kumpoteza Seneta wao. Nilikuwa na bahati kuenda kumtembelea kwa hospitali mara mbili wakati wa mwisho ikiwa jumatatu wiki iliyopita kule Mombasa, nikamuona, tukasamilimiana na tukazungumza. Alikuwa na matumaini makubwa kwamba atapona na atarudi katika Seneti lakini mapenzi ya Mwenyezi Mungu, alichukua roho yake. Ninamshukuru mwenyezi Mungu kwa kutupa Boy Juma Boy, tukajuana naye na tukafanya kazi naye katika Seneti hii. Bw. Naibu Spika, vile Sen. Boy Juma Boy amesifiwa na wengi, ni wachache sana walio kuwa na tabia kama ya Boy Juma Boy. Alikuwa anahisi maslahi ya wengine kuliko yake. Alikuwa tayari kukusaidia ukiwa na shida. Nakumubuka akihudhuria kila mikutano. Kama Seneta wa kamati za Seneti hakukosa mikutano. Akikosa mkutano ilikuwa ni wazi kwamba hayuko mjini. Alikuwa ni mtu wa kutegemea katika Kaunti ya Kwale. Kazi yake itakumbukwa kwa siku nyingi haswa kazi aliyofanya katika ugatuzi na kusaidia Kaunti ya Kwale kutekeleza majukumu yao kwa wenyeji wa Kaunti ya Kwale. Katika Seneti, tunamkumbuka Boy Juma Boy kama mtu mcheshi aliyependa wenzake na mwenye kusema ukweli na hata kama hungekuwa huipendi, angekuambia ukweli. Kwa hivyo sisi kama Maseneta tutamkumbuka ndugu marehemu Sen. Boy Juma Boy kwa ucheshi, upendo na urafiki wake. Lakini Mwenyezi Mungu alimpenda zaidi ndiyo akachukua roho yake. Tunamwomba aiweke mahali pema panapostahili."
}