GET /api/v0.1/hansard/entries/725400/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 725400,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/725400/?format=api",
"text_counter": 91,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Elachi",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13115,
"legal_name": "Beatrice Elachi",
"slug": "beatrice-elachi"
},
"content": "Asante Bw. Naibu Spika. Kwanza nakushukuru na wale wote waliokwenda kule Vanga kutuwakilisha kumsindikiza ndugu yetu marehemu Sen. Boy Juma Boy kwa safari yake ya mwisho. Pia natuma rambi rambi zangu kwa familia yake, hasa mama na watoto. Nawaambia ya kwamba safari hii ni ya kila mtu. Sisi kama Maseneta tumwombe Mungu kwa sababu huyu ni ndugu wetu wa tatu aliyetuacha kwenda katika maisha ya mbinguni. Lakini ya muhimu ni kukumbuka yale marehemu Sen. Boy Juma Boy alisimamia na yale aliyopigania kwa watu wake wa Kwale. Tunawaambia ndugu, dada na mama wetu kule Kwale kwamba tuko pamoja nao kwa msiba huu. Tunajua kwamba matunda yale marehemu Sen. Boy Juma Boy angependa kuona yatatekelezwa. Tunaomba serikali ya kaunti ikumbuke yale maswala alikuwa anapigania na iwasaidie watu wa Kwale ili wawezi kuona mabadiliko aliyotaka marehemu Sen. Boy Juma Boy. Mwisho kabisa, sisi tujiulize; sisi tutakumbukwa vipi tunapo mkumbuka marehemu Sen. Boy Juma Boy. Kwa hayo machache, Bw. Naibu Spika, tunamwomba Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu Sen. Boy Juma Boy mahali pema peponi."
}