GET /api/v0.1/hansard/entries/725410/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 725410,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/725410/?format=api",
    "text_counter": 101,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Asante sana Bw. Naibu Spika. Mimi pia nataka kuomboleza na Maseneta wenzangu kifo cha ndugu yetu Boy Juma Boy. Kifo chache ni cha watu wa Kijiji cha Rasini, watu wa Kwale, watu wa pwani na Wakenya wote. Ndugu yetu marehemu Boy Juma Boy alikuwa na sisi hapa kama Seneta. Nataka kuwatolea mshangao kwamba watu wawili waliopendana katika hili Bunge walikuwa marehemu Boy Juma Boy na marehemu Otieno Kajwang. Cha kushangaza ni kuwa wote walikuwa wanaketi kona moja. Mwenyezi Mungu ana mipangilio yake. Sasa hivi, marehemu ndugu yetu amekwenda kukutana na mwenzake marehemu Otieno Kajwang. Najua Mwenyezi Mungu amerehemu roho zao. Bw. Naibu Spika, mengi yamesemwa juu ya marehemu Boy Juma Boy. Wamesema kuwa alikuwa mcheshi si ndani tu ya Bunge bali hata nje. Mimi ni mmojawapo wa wale watu waliokuwa karibu sana naye hasa akiwa anachangia mjadala hapa ndani ya Bunge uliohusika na mambo ya Kwale. Ndugu yangu Boy Juma Boy alikuwa mkakamavu zaidi. Alikuwa mtu aliyetaka kuona kwamba vile alivyosema ndivyo watu wa Kwale wangesema wakiwa pamoja hapa. Alikuwa mtaalamu wa lugha ya Kiswahili. Sisi sote tukiwa hapa ndani ya Bunge, tulikuwa tunafurahi alipokuwa akiongea. Ijapokuwa mimi natoka pwani, yeye alikuwa ananishinda kwa utaalamu wa kuongea lugha ya Kiswahili. Alikuwa na mifano tofauti tofauti. Natumai tunakumbuka mfano wake wa simba na tumbiri. Mpaka leo najaribu kutafakari nini alichokuwa analenga ndugu yangu Boy Juma Boy. Alisema kuwa tumbiri alikuwa amepanda juu ya mchongoma. Alikuwa amedungwa na miiba na damu ilikuwa inatoka. Alipoangalia chini, alimwona simba akilamba ulimi wake huku amefurahi. Simba alimwuliza; “unaona nini huko mbele?” Tumbiri alimjibu kuwa mbele hakukuwa na neno wala shida lakini shida ilikuwa pale chini. Kwa hivyo, ni vyema tutafakari mifano kama hiyo; kwamba kuna leo na kesho. La ziada zaidi ni kwamba juzi, kama miezi mitatu iliyopita, ndugu yangu alinialika nyumbani kwake Vanga ili niongee na watu wake na kuwaeleza kinagaubaga kazi za Seneti. Nilishikana naye tukaenda pamoja mpaka Vanga kisha tukafululiza hadi Kijiji cha Rasini ambako mji wa marehemu Mzee Juma Boy uko. Tulifanya mkutano wa kufana sana. Sikujua kuwa nitarudi huko baada ya miezi miwili kwenda kumzika ndugu yangu katika kaburi--- The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate"
}