GET /api/v0.1/hansard/entries/725415/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 725415,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/725415/?format=api",
    "text_counter": 106,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Chiaba",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 3,
        "legal_name": "Abu Mohamed Chiaba",
        "slug": "abu-chiaba"
    },
    "content": "Bw. Naibu Spika, asante kunipa fursa hii kuungana na wenzangu hapa kutoa rambirambi zetu za dhati kuhusu kifo ambacho kimetunyang’anya ndugu yetu tuliyemtegemea kwa mambo mengi sana. Nilibahatika kuwa naye katika Bunge la Taifa kwa miaka 10 na nilimtambua sana kama kiongozi wa kitaifa. Vile vile, nilifurahi mimi na yeye tulipokuja hapa katika Bunge la Seneti. Nakumbuka tumesafiri naye mara nyingi sana. La muhimu ni kwamba tulisafiri pamoja kwenda katika miji mitakatifu ya Mecca na Medina. Yeye alikuwa mtu aliyekuwa na imani kubwa kuweza kutekeleza wajibu wake kama Muislamu. Nilipata fursa ya kumtembelea marehemu siku ya Ijumaa iliyopita katika hospitali ya Aga Khan. Alifurahi aliponiona kisha tukafanya maombi. Nilimwombea apone haraka iwezekanavyo. Ya Mungu ni mengi na Jumapili alienda zake. Mwenyezi Mungu aiweke roho yake peponi. Ndugu zetu wote waliobakia wakiwemo watu wa Kwale, watu wa pwani na Wakenya kwa jumla, Mungu awape subira na imani."
}