GET /api/v0.1/hansard/entries/725540/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 725540,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/725540/?format=api",
"text_counter": 231,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Muthama",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 96,
"legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
"slug": "johnson-muthama"
},
"content": "Bw. Spika wa Muda, Hoja hii ina maana sana. Ningeomba muda uongezwe. Kutoka tunyakuwe Uhuru wetu, nchi hii haijawahi kukumbwa na matatizo kama yanayotukumba sasa. Serikali ya hayati Mzee Kenyatta haikuwa na migomo ya madaktari. Serikali ya Rais Moi, ingawa ilikuwa na shida nyingi, haikuwa na migomo ya madaktari. Serikali ya Rais Kibaki, pia haikuwa na migomo ya madaktari. Lakin leo, kuna mgomo wa madaktari. Bw. Spika wa Muda, unavyotuona sisi hapa tukiwa tumevalia tai na suti, tunakanyaga zulia nyekundu na tuna maji ya kunywa mbele yetu. Watoto na wajukuu wetu wakiwa wagonjwa, wataenda hospitalini. Nimesima hapa kuzungumza juu ya mwananchi wa kawaida. Leo, Rais Kenyatta akiwa mgonjwa, hataenda hospitalini. Madaktari wataenda kwake nyumbani kumuhudumia. Pia mke wake na watoto wake wakiwa wagonjwa, hawataenda hospitali, madaktari wataenda nyumbani kuwahudhumia. Akina mama wanaojifungua wanahisi uchungu sana na watoto wao wanakufa kwa sababu wanakosa usaidizi wa madaktari. Wengine wanakufa kutokana na majeraha wanaposubiri kulazwa hospitalini. Nchi yetu imekosa mwelekeo. Bw. Spika wa Muda, wewe kama daktari unajua ni pesa ngapi Serikali ya Rais Uhuru Kenyatta ilitumia kumfanyia kampeini Amina Abdalla ili ateuliwe kama Mwenyekiti wa Muungano wa Afrika (AU). Mambo haya yanafanyika--- The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate"
}