GET /api/v0.1/hansard/entries/725558/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 725558,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/725558/?format=api",
"text_counter": 249,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Muthama",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 96,
"legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
"slug": "johnson-muthama"
},
"content": "Bw. Spika wa Muda, mazungumzo yangu yanakwenda sambamba na maneno uliyoyasema na pia yale Sen. (Dr.) Khalwale aliyesema. Nakodolea macho na kuinyooshea kidole ofisi iliyo na mamlaka; ofisi ya Rais wa nchi ya Kenya. Mambo yakifika njia panda tulipo, nalihakikishia Bunge hili na Wakenya kwamba niko tayari kulipa bei yoyote hata kama ni kufungwa jela, maisha au lolote lakini nizungumze ukweli. Ikiwa daktari hawafanyi kazi na waziri na katibu hawana nguvu, ni nani mwingine nitakayemuuliza atuambie shida ya madaktari ni gani, kama sio Rais. Kama yuko katika ile ofisi na hawezi kuulizwa swali, basi Kenya iko katika hali mbaya, hata hatujui tuko wapi. Ni jukumu la Rais kuona kwamba madaktari wameshughulikiwa. Walishuhudia Magavana wakilazimishwa kununua mitambo ya Kshs38 billion huko wakiwa hawana mshahara. Pia juzi, wizara hiyo imehusishwa na kashfa ambapo ilipoteza kiasi kikubwa cha pesa ilhali madaktari hawana pesa. Wakenya wana haki kupata haki yao. Mheshimiwa Uhuru Kenyatta, waambie Wakenya watatibiwa namna gani na mgomo wa madaktari utaisha lini? Bila hayo hatunyamazi, tutazungumza hadi nchi na mbingu ishikane."
}