GET /api/v0.1/hansard/entries/725596/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 725596,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/725596/?format=api",
"text_counter": 287,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Asante sana, Bw. Spika wa Muda. Naunga mkono Hoja hii. Ningependa kuzungumza kuhusu mgomo wa madaktari, wewe ukiwa mmoja wa madaktari shupavu humu nchini. Katika historia Kenya, ni mara ya kwanza mimi kushuhudia madaktari wakigoma siku zisipopungua 75. Ni aibu ya hali ya juu kwamba wananchi wanaweza kukosa kutibiwa na wengine wakafa bila Serikali yao kuwangalia. Nchi isiyo angalia maslahi na afya ya wananchi imekosa mwelekeo. Nasema hivi kwa sababu ya uzembe kama huu. Unapata ya kwamba madaktari wanadai haki yao. Huwa wanalipwa mishahara duni ilhali kazi wanayo ifanya ni ngumu sana. Kuna umuhimu wa kuweza kuangalia ama kuchunguza ni kwa sababu gani madaktari wetu wamechukua hatua hiyo. Mimi mwenyewe nilikuwa Judge wa hiyo korti, lakini cha kushangaza ni kwamba daktari ni mtu ambaye amesoma kwa miaka mingi na anaelewa anacho kifanya. Kufunga daktari sio kufunga ugonjwa. Ukimfunga daktari, ule ugonjwa unaendelea kutapakaa kwa mwili wa binadamu. Ukimuachilia daktari, ndio anaweza kutibu. Daktari amengonga hodi na ni lazima tufungue mlango na tuulize ni kwa nini madaktari wetu wamegoma. Jambo la kusikititisha ni kwamba katika korti yetu ya wafanyakazi wameanza kuangalia zaidi, the law of evidence and the Criminal Procedure Code katika lugha ya kiingereza. Tunasema kwamba, katika mambo ya wafanyakazi inafaa kuwe na uhusiano mwema kati ya tajiri na muajiriwa wake hivi kwamba wanaweza kukaa chini na wakaongea. Zamani nikiwa jaji tulikuwa tuna mwita tajiri na yule mfanyikazi na wote wana kuwa sawa mbele ya korti na inakuwa ni lazima wasikizazane na waandikishe masikizano yao katika korti. Hapa kuwa na ushindano kama uliopo hivi sasa. Hata ninashangaa kuona kwamba hakuna mbinu zozote zina tumiwa kumuita yule tajiri an muajiriwa ili waweze kuongea. Hilo ni jambo la kusikitisha, hususan ukiangalia zaidi, Bw. Atwoli aliongea habari ya Katibu Mtenda kazi, Bw. Muraguri; kwamba alikosa kuenda katika mazungumzo, na Bw. Mailu akamtetea kwamba mtu mmoja The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate"
}