GET /api/v0.1/hansard/entries/725598/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 725598,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/725598/?format=api",
"text_counter": 289,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "hawezi kufanya mazungumzo yasiendelee. Lakini ujue kwamba huyu ni Katibu Mtendakazi wa Wizara ya Afya. Kwa hivyo, ni jukumu lake yeye kukaa katika yale mazungumzo kuhakikisha ya kwamba yale matakwa ya madaktari yame sikizwa vilivyo, hususan mishahara yao na matakwa mengine. Ni lazima Bw. Mailu na Bw. Muraguri waelewe ya kwamba Kenya ina bahati kuwa na Bw. Atwoli ambaye ana tambulika katika dunia nzima kwa kutetea haki za wanfanya kazi. Ni mtu aliye na taaluma na hawezi kuongea uwongo. Inafaa wamsikize. Ninaambiwa kwamba nabii hana heshima kwao lakini kwa heshima ya wananchi waTaifa la Kenya, nina waomba Bw. Muraguri na Bw. Mailu wamsikize ili kusitisha huu mgomo. Bw. Spika wa Muda, tumesema kwamba mambo kuhusu afya ya shughulikiwe katika serikali za kaunti. Hiyo ndiyo tulipitisha na tukasema kwamba kitengo cha afya Kibaki katika serikali za kaunti. Hivi sasa, tunaona Serikali kuu iki walazimisha kuandika mikataba tofauti tofauti ili wachukue vifaa katika hospitali. Ni kama hii Serikali ya Jubilee haitaki kuacha kitengo cha afya kwenye mikono ya magavana kwa sababu wao ndio wanajua hali ilivyo mashinani. Waswahili husema kwamba anaye vaa kiatu ndiye anayejua vile kinavyouma."
}