GET /api/v0.1/hansard/entries/725599/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 725599,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/725599/?format=api",
"text_counter": 290,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Njoroge",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13158,
"legal_name": "Ben Njoroge",
"slug": "ben-njoroge"
},
"content": "Asante Bw. Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii ili ni weze kujiunga na wenzangu kujadili Hoja hii. Nikiunga hii Hoja mkono, ningependa kusema kwamba ni jambo la kusikitisha kuona kwamba leo hii madaktari wamegoma na hawawezi kutekeleza wajibu wao wa kutibu wagonjwa katika hii nchi ya Kenya. Pia ni jambo la kusikitisha kwamba madaktari wamefungwa gerezani kwa sababu ya kutotii sharia ya korti. Hili ni jambo ambalo Wakenya wanafaa waelewe kwamba kuna sheria katika nch ihii. Mara nyingi tumeona watu wakipuzilia mbali maagizo ya korti na kufanya mambo kivyao. Bw. Spika wa Muda, itakumbukwa kwamba hivi juzi nilikuwa na shida baada ya kampuni ambayo nilikuwa nikihusika nayo kufanya biashara kupuuza maagizo ya korti na kunishambulia kazini mwangu kule Naivasha. Wakati niliona Mkurungenzi Mkuu wa Vivo Energy, Polycarp akinishambulia, nikakumbuka yale ambayo madaktari wanapitia kwa kupuuza maagizo ya korti. Mkurugenzi huyu hakukatazwa na korti kuja mahali nilipo kuwa ninafanyia kazini. Kwa hivyo, ninaushahidi kwamba watu wamekuwa wakipuuzilia mbali maagizo ya korti na ninafikiria ni vizuri Wakenya waelewe kwamba ni lazima sheria izingatiwe na kila mtu bila kufikiria kwamba kuna yeyote anayeweza kuwa juu ya sheria. Huu mgomo wa madaktari umeingiliwa na wanasiasa na kufanya huu mgomo kuendelea kwa muda mrefu zaidi. Siasa inapoingizwa kwa jambo fulani, ni lazima patokee shida. Ni jukumu la Serikali kuhakikisha ya kwamba Sheria inadumishwa hata kama watu wanajaribu kuingiza siasa katika maisha ya wanadamu. Ninaunga Hoja hii mkono nikisema kwamba nilazima wakenya watii maagizo ya korti kwa sababu korti ziko na zitakuweko na ni lazima tufuate maagizo yao. Asante."
}