GET /api/v0.1/hansard/entries/725602/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 725602,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/725602/?format=api",
    "text_counter": 293,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Ingekuwa vyema kama Serikal ingejitokeza na kuzungumzia jambo hilo. Sio vyema kununua mashine na kupeleka kwenye hospitali. Vifaa vinavyo pelekwa hospitali lazima viwe vya Kisasa na ni lazima kuwekwe mikakati ili hospitali hizo ziweze kuwahudumia wagonjwa. Bw. Spika wa Muda, katika nchi zingine zilizo endelea, huduma kwenye hospitali zao ni za hali ya juu sana. Nchi kama ya Uingereza, viongozi wao hupata huduma za matibabu katika hospitali za serikali. Kwa hivyo, madaktari wanapotaka sekta ya afya iboreshwe, wana zungumzia jambo njema. Korti zetu hazina huruma wanapo wahukumu madaktari. Korti zimeingilia mambo yote na Tume Huru ya Uchaguzi (IEBC) haiwezi kufanya kazi kwa amani. Majaji hawaoni Wakenya na kwa hivyo wanafaa kuona kuwa kila chama sasa kina angazia uchaguzi. Hata watoto wa Kenya wanajua kuwa kuna uchaguzi. Leo ndiyo siku ya mwisho ya wananchi kujisajili kupiga kura. Sina uhakika kama Tume ya IEBC imeongeza muda huo lakini korti zetu hazifanyi haki. Madaktari wanafungwa jela na hilo sio jambo njema. Wakati wa mwisho wa Wakenya wanao pigania haki zao kufungwa ilikuwa wakati wa ‘multi-partism’na wakati wa kupigania Uhuru wa Kenya. Madaktari wanapigania uhuru wa Wakenya kwa kutaka sekta ya afya iboreshwe."
}