GET /api/v0.1/hansard/entries/726821/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 726821,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/726821/?format=api",
"text_counter": 403,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Bady",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1612,
"legal_name": "Bady Twalib Bady",
"slug": "bady-twalib-bady"
},
"content": "Ahsante sana, Bi. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii nami niweze kuizungumzia Ripoti ya Rais. Ninaiunga mkono Ripoti hii. Ninakubaliana na Rais kwamba watu wote wanatakiwa kuishi kwa umoja. Usalama wa nchi huadhirika kwa njia nyingi. Ndiposa tunazungumzia usalama juu ya lishe bora. Tunazungumzia usalama juu ya elimu. Pia tunazungumzia usalama juu ya uadui wa nje na ndani ya nchi. Bi. Naibu Spika wa Muda, juzi wewe ulikuwa mkali sana ulipokuwa ukizungumzia hali ilivyokuwa kule Baringo. Bado, pia tunasema vilevile; kwamba, ni jukumu la viongozi walioteuliwa katika sehemu zile kuona jinsi watakavyowajibika ili kudumisha usalama katika maeneo yao, wakishirikiana na viongozi wengine. Hata hivyo, kunyoosha kidole cha lawama kwa mtu mmoja haiwezekani kwa sababu Rais pekee hawezi kupigana vita hivi pasipo na ushirikiano. Baadhi ya watu katika nchi hii tunaona kuwa mambo mengi ambayo yanasababisha shida ni kusahaulika kwa baadhi ya sehemu za nchi hii tunapoweka miundo musingi muhimu. Mhe. Nyenze alizungumzia shida za maji katika sehemu kadhaa za Kenya. Mimi leo ninazungumza kwa uchungu kwa sababu katika eneo langu la Jomvu, katika Kaunti ya Mombasa, muda huu wote kuanzi wakati tulipopata Uhuru, mwananchi kupata maji ni kama kuona dhahabu. Katika sehemu nyingi watu hupigana vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa ajili ya uhaba wa maji. Maji ni bidhaa adimu. Watu hupigana kwa ajili ya maji ndiyo wanyama wao waweze kupata maji ya kunywa na wao wenyewe waweze kupata maji yatakayowawezesha kujikimu. Je, inakuwaje binadamu anakosa maji katika sehemu anakoishi? Ninazumgumza nikiwa Mbunge. Mbali na kuiunga mkono taarifa ya Rais, kuna vitengo kadhaa, kama vile Coast Water Services Board na Mombasa Water and Sewerage Company, ambavyo viko katika Serikali ya Taifa. Tukiangalia, kuna ufadhili mkubwa sana ambao ulipatikana kutoka World Bank ili kuweza kupitisha mabomba kutoka chemichemi ya Mzima Spring kuleta maji mpaka sehemu za Mombasa, lakini mpaka leo tunayaona mabomba yale yakitembea barabarani. Yamekuwa mabomba ya rangi ya kibichi. Yamekaa sana, hakuna kazi yoyote ambayo imefanyika katika muda wa mwaka mmoja na nusu kufikia sasa ilhali hali haijabadilika na watu wanaendelea kupata shida. Ninamsihi Mhe. Rais kwamba tulifuatilie jukumu hili muhimu ili tuweze kuona kwamba wananchi wanaweza kupata bidhaa hii adimu. Ni muhimu Serikali ishughulikie hali hii kwa sababu wananchi wanaendelea kuumia. Hatuwezi kuumauma maneno tukisema kwamba kila kitu kiko sawa ilhali mambo mengine hayako sawa. Ni muhimu tuwajibike na kuona kwamba maji yanapatikana katika sehemu zetu. Nikiwa kwenye Bunge la Taifa, ninataka ninukuliwe nikisema kwamba hali hii imenitamausha mimi binafsi nikiwa Mbunge wa Jomvu. Ninaisihi Serikali tushirikiane pamoja ili maeneo ya Miritini, Jomvu Kuu na Mikindani yaweze kupata maji ndiyo wakazi wa sehemu zile waweze kuishi vizuri. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}