GET /api/v0.1/hansard/entries/726822/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 726822,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/726822/?format=api",
"text_counter": 404,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Bady",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1612,
"legal_name": "Bady Twalib Bady",
"slug": "bady-twalib-bady"
},
"content": "Ninamuona Mhe. Sakaja akipiga chini vizuri kwa kuashiria kuwa anakubaliana nami kwa sababu mkwewe na mke wake wanatoka Miritini, ambayo iko katika sehemu yangu ya uwakilishi Bungeni. Leo mama mkwe wa Mhe. Sakaja hana maji. Kwa hivyo, ninataka Serikali ya Mhe. Uhuru Kenyatta ijue kwamba mimi niliyoko katika muungano wa National Super Alliance (NASA), ambao imeshanaswa; na ndugu yangu Mhe. Sakaja, ambaye yuko katika muungano wa Jubilee, sote tunapata shida katika sehemu hiyo. Ninaomba Rais aingilie kati aone jinsi wananchi watakavyoweza kupata maji. Mwisho, ufisadi hauwezi kuisha ikiwa vita hivi tutamwachia Rais pekee. Ni lazima tupigane vita hivi pamoja. Ni lazima tushirikiane. Tusingojee kumumwagia Rais lawama na kusema ameshindwa kumaliza ufisadi. Hatuwezi kusema Rais amefeli kama mwenye kupewa na mwenye kuchukua hongo hawatashirikiana kwenya kitendo cha ufisadi. Kwa hivyo, ni lazima tuhakikishe kwamba tunaidhibiti hali hii pamoja; kama kunavyofanywa katika nchi nyingine, ambako ufisadi ni kama donda sugu ambalo haliwezi kukubalika. Nilitembea katika nchi ya Rwanda, ambako mambo ya ukabila hayaruhusiwi kabisa. Katika nchi ya Rwanda, ukiwa ndani ya gari na uvute sigara halafu urushe ncha ya sigara chini, dereva wa texi anaweza kukuripoti kwa polisi. Hilo jambo linamaanisha wote wameungana pamoja kuweka nchi yao safi na kuweka kando kwa ufisadi. Ni muhimu Wakenya tuige huo mfano ili tuweze kumkosoa Rais kwa mambo mengine, lakini si kuhusu mambo ya ufisadi. Ni jukumu letu sote kwa pamoja kuijali nchi yetu. Ni jukumu la Serikali iliyoko na wale walioko upande wa Upinzani, pamoja na wananchi, kuhakikisha kwamba nchi yetu iko katika hali nzuri. Kwa hayo machache, ninarudisha shukrani kwa Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii ili namimi niweze kuchangia mjadala juu ya Ripoti ya Rais."
}