GET /api/v0.1/hansard/entries/726892/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 726892,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/726892/?format=api",
    "text_counter": 474,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Wanyama",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 1076,
        "legal_name": "Janet Nangabo Wanyama",
        "slug": "janet-nangabo-wanyama"
    },
    "content": "Ningependa kuongea kuhusu ufisadi katika nchi yetu ya Kenya. Ni kweli kwamba ufisadi umekita mizizi katika nchi yetu ya Kenya, lakini hiyo haimaanishi kwamba ufisadi umeletwa nchini na Mhe. Rais. Ufisadi unapatikana hata kwenye nyumba zetu, na hata makanisani. Ningependa kuishukuru Serikali kwa kuhakikisha kwamba wale wanaopatikana na makosa ya ufisadi wanachukuliwa hatua kulingana na sheria. Kwa sababu ya ugatuzi, katika nchi yetu kumekuwa na changamoto chungu nzima. Utaona kwamba watu ambao wameajiriwa na viongozi wenzetu wamejipatia utajiri kwa njia isiyo halali. Ningependa kusema kwamba sisi, kama viongozi, ni lazima tushikane bega kwa bega kuhakikisha kwamba tunapambana na ufisadi katika inchi yetu ya Kenya."
}