GET /api/v0.1/hansard/entries/727054/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 727054,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/727054/?format=api",
    "text_counter": 139,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mositet",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 608,
        "legal_name": "Peter Korinko Mositet",
        "slug": "peter-korinko-mositet"
    },
    "content": "Asante sana, Bw. Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii ili niweze kuungana na Seneta wenzangu ambao wametoa rambirambi zao kwa niaba ya kaunti zao. Natoa rambirambi zangu na za kaunti yangu kwa familia ya rafiki wetu Gov. Nderitu Gachagua, jamii yake na Kaunti ya Nyeri yote. Gov. Nderitu Gachagua aliweza kuingia siasa wakati kulikuwa na watu ambao walijulikana kuwa shupavu sana kama vile Mheshimiwa Matu Wamae. Wengi wetu tulikuwa vijana tulifurahi sana kuona ya kwamba kiongozi chipukizi kwa jina la Nderitu Gachagua alipigania kiti cha Mathira na kushinda. Kwa hivyo, ushujaa wake uliweza kuonekana mapema akiwa kijana. Alikuwa mtu ambaye hakuwa na uoga hata kidogo. Wakati alipohitajika kufika mbele ya Seneti kwa sababu wabunge wa kaunti walikuwa wanataka apoteze kiti chake cha ugavana, ninakumbuka Sen. (Dr.) Khalwale akisema kuwa Gov. Nderitu Gachagua akubaliwe aketi chini. Yeye aliona ni kama Sen. (Dr.) Khalwale alidhani yeye ni mnyonge na kumuonea huruma. Kwa kweli Gavana Gachagua alisimama pale siku mbili akiwa na ujasiri mpaka tuka ikamilisha ile Hoja. Nalipongeza Bunge hili kwa sababu hata baada ya hayo, aliweza kuachiliwa, hakua na hatia. Pia mliona kwamba aliweza kujitetea na kuonyesha kwamba alikuwa na uongozi bora. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate"
}