GET /api/v0.1/hansard/entries/727060/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 727060,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/727060/?format=api",
"text_counter": 145,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "inafanywa kwa bei ya juu sana. Inabdii watu watafute nafasi za kwenda nje kwa matibabu ya bei nafuu. Kuna umuhimu wa Serikali ya Jubilee kufanya bidii na kutenga pesa za kutosha kuona ya kwamba Wakenya hawana haja ya kutibiwa katika hospitali za bei ghali huko ng’ambo, bali humu nchini. Hospitali zilizoko India, South Africa na kwingineko zinaweza kutengenezwa hapa. Ikifanyika hivyo, madaktari wetu wataweza kutibu Wakenya. Bunge hili lilimpatia nafasi marehemu Gachagua kujitetea hapa. Alifanya vilivyo na hatimaye akapatikana bila hatia. Hatutaki kusema tuko watakatifu ama tuna msifu kwa sababu amefariki. Ndungu yake jana alisema ya kwamba hawataki watu watakao msifu marehemu Gachagua kwa sababu ame aga dunia. Wale wapinzani wake wakome kwamba wanaweza kusema mambo mazuri wakati huu amekwenda. Alisema mambo ya mtu yasemwe akiwa hai. Kwa mfano, kama Seneta Kagwe ni mtu mzuri, sema sasa. Usingoje mtu akifa halafu uje useme baadaye. Bw. Spika wa Muda, kwa hayo machache naungana na wakaazi wa Kaunti ya Nyeri, familia na Wakenya wote kwa ujumla kwa kumpa pole mjane, ndugu na marafiki. Tunaomba Mwenyezi Mungu airehemu roho ya marehemu Gachagua mahali pema peponi."
}