GET /api/v0.1/hansard/entries/727079/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 727079,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/727079/?format=api",
    "text_counter": 164,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Wangari",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13123,
        "legal_name": "Martha Wangari",
        "slug": "martha-wangari"
    },
    "content": "Asante sana, Bw. Spika wa Muda. Nachukua nafasi hii kwa niaba yangu, familia yangu na wananchi wa Gilgil na Nakuru kwa ujumla kutoa rambi rambi zangu kwa familia ya mwenda zake Gavana Gachagua na Sen. Kagwe. Tunaomboleza nao. Tunakumbuka kuwa sio muda mrefu umepita tangu tuwe naye hapa. Ingawa alikuwa anaugua, alijikakamua na kujikaza kisabuni kufika hapa kujibu maswali yaliyomkumba. Kifo chake kimetokea wakati kuna mtafaruku na shida kuhusu madaktari nchini. Ugonjwa wa saratani umeendelea kuua watu wengi wakiwemo watoto na akina mama. Kama hakuna wauguzi watu wa hadhi ya chini wanaumia sana kwa sababu hawawezi kupata matibabu kwenye nchi za nje. Hawawezi kwenda Uingereza, India au mahospitali za kibinafsi kwa sababu ya gharama kubwa. Kila wiki tunaalikwa kwa michango ya pesa ili kupeleka ng’ambo watu wanaougua ugonjwa wa saratani kupata matibabu. Huu ni mwaamko kwa serikali kuhakikisha kwamba tumetatua shida hii ya madaktari na wauguzi. Wasikilizane ili tuokoe maisha ya wale wanaougua na familia ambazo zimetumia pesa zao zote kutafuta matibabu. Vile vile, naunga mkono Sen. (Dr.) Khalwale. Kulingana na kipengee cha 179 cha Katiba, Gavana aliyechukua mahali pa marehemu Gavana Gachagua ---"
}