GET /api/v0.1/hansard/entries/729400/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 729400,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/729400/?format=api",
"text_counter": 339,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Machage",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 179,
"legal_name": "Wilfred Gisuka Machage",
"slug": "wilfred-machage"
},
"content": "Bw. Spika, kwa historia ya Waisraeli kulitokea wafalme kadhaa. Mmoja aliyeitwa Suleimani aliulizwa na Mungu yuataka nini kwa sababu alikuwa amemtendea wema. Hakutaka almasi, dhahabu, lulu wala wanawake. Alisema, ninataka hekima. Basi alitambuliwa kuwa mfalme mmoja aliyeishi kwa hekima. Ni kweli kuwa ukiwa mtawala katika cheo hicho cha rais wa nchi ombi moja ambalo lastahili umwombe Mungu akutunukie wazo na akili ndio kama Suleimani uwe na hekima. Ni rahisi sisi tukiwa hapa nje kuona mpira ukichezwa kama vile sisi katika upinzani wakati mwingine hudhani. Mmoja wetu hupenda kusema: “Fulani ana mpira, Wetangula na mpira, fulani ameushika, mara bao! Kweli wewe wasema hivyo, lakini ingia kwa uwanja ukaucheze huo mpira, utoe changamoto kama zile na kisha ufunge bao ambalo limo mawazoni mwako. Mhe. Rais alitoa hotuba iliyoonyesha machache ambayo yametekelezwa na Serikali yake katika hii nchi kwa muda wa miaka minne. Si sote ambao tumeridhika Kenya nzima lakini ukweli ni kwamba amejaribu kutekeleza mengi. Hotuba yake iliangazia miradi ambayo inatekelezwa wakati huu na ile ambayo itatekelezwa siku za usoni. Lakini swali letu ni hili: Je, haki imetendeka kwa kila mtu nchini? Mkoloni alianza kuijenga reli kuanzia Mombasa ikielekea Kisumu. Mji wa Nairobi ulikuwa kituo kilichokuwa na maji baridi. Kituo hiki kikaimarika na kuwa jiji la The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate"
}