GET /api/v0.1/hansard/entries/729402/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 729402,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/729402/?format=api",
    "text_counter": 341,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Nairobi kama tunavyojua leo. Mkoloni alitengeneza barabara zakuingia vitongojini kule Rumuruti na Laikipia. Hata hivyo, alisau kuimarisha barabara za Mandera na Kuria kwa sababu mawazo yake yalikuwa ya kutawala na kupata ardhi yenye rutuba na madini. Basi reli ilijengwa kuanzia Mombasa hadi Kisumu bila kufikiria barabara za sehemu zingine. Hata sasa baada ya miaka 50 ya Uhuru, reli mpya au SGR inafuata mkondo huo wa zamani. Reli mpya imetoka Mombasa, ipitie Nairobi, Naivasha hadi Malaba. Wengine ambao tunaachwa tutasaga meno na kusononeka kwa sababu sisi pia ni Wakenya. Twataka tusikie mipango ya reli ikituhusisha. Kwa mfano, kama reli itafika Naivasha, basi ilikeweze kupitia Kisii, Migori, hadi ifike Sirare na Isebania mpakani kuelekea mji wa Mwanza, Tanzania. Na sisi tujisikie kuwa pia, tuna Uhuru na haki kutendeka kwetu. Sisi hukuza mahindi, sukari, njugu karanga, mtama na pia tuna madini kama dhahabu na kadhalika. Sisi tutawekwa darubini lini? Twataka kusikia mipango ya maendeleo katika kaunti zetu. Hata kwa wale ambao watakuja siku za usoni, sijui kama ni akina Sen. Wetangula na wengine ambao “wananaswa naswa” kidogo katika chama cha NASA, lakini tunataka kusikia mipango yao hata wakati wa kampeni ni ipi. Je, wana mipango ya kujenga reli kule Kuria, Migori na Kisii? Bahati ya Mkuria ilienda wapi? Je, barabara zimejengwa? Kulikuwa na mipango ya kujenga 10,000 kilomita za barabara. Zimelimwa lakini zimesambazwa namna gani? Serikali iliyopita ililima kilomita tano tu ya barabara kutoka Isebania-Ikerege-Kehancha-Witende. Barabara ya kilomita hamsini na sita na ikaachwa hapo na kusahaulika. Pia barabara ya kupitia Isebania-Sirare-Jamtiro-Ntimaro iende kuungana na bonde la ufa, ni yenye manufaa na mazao mengi ya kilimo. Hakuna ambaye anasema au kuweka mambo kama haya katika mipangilio yao. Ninaamini labda mzee hajaambiwa. Sasa namwambia nikitumia Bunge hili kwamba ingawa twashukuru kwamba kuna mipango imewekwa kamilifu ya kujengwa shule, zahanati na hospitali za wilaya na mbinu za kuinua utali na kadhalika. Wakati mwingi unawezakuangua kicheko usikiliza wanayotaka kutekeleza. Hii ni kwa sababu hakuna la maana utakaloliona katika hotuba kuhusu kaunti zingine. Serikali ya Mhe. Rais Kenyatta imefanya mambo mengine mazuri. Sifa twazitoa lakini afungue macho pia kwa sababu Kenya ni kubwa. Tuna makabila 43 hapa nchini. Tuna kabila za Wahindi ambao ni Wakenya. Kwa hivyo, hapa nchini tuna makabila zaidi ya 45. Hizo ni nyumba zake zakulinda. Sisi sote tunataka haki itekelezwe kwa kila Mkenya. Makabila mengine ni makubwa na mengine madogo. Lakini tunataka haki kwa kila mtu. Wengine wasije wakafikiria ya kwamba kwa sababu mimi Mungu kaninyima kizazi cha kutosha, basi sitambuliki katika nchi hii. Mwingine kasema kwa sababu mimi Mungu alinitunukia kizazi cha kutosha nikikalia ratili ya uchaguzi, basi Rais atatoka hapa na mimi ndiye wakufikiriwa zaidi. Twajua Rais mstaafa Bw. Moi alitoka kwa kabila ndogo ya Watugen. Hakuna kabila inaitwa Wakalenjin, lakini akawaita hivyo akajazajaza chembe kwa sababu huwezi kupika chembe moja ya mahindi. Lazima ukusanye makabila madogomadogo. Kuna wakati ametawala hii nchi bila kabila ya Mjaluo, Mkikuyu na akapita kura yake kwa sababu alitambua umuhimu wa kuwepo kwa jamii ndogondogo na hiyo ndiyo siri. Sasa hivi tunaangaza macho yetu kwa uchaguzi. Ninatoa hisia kwa viongozi na Rais wa nchi hii. Hesabu sasa zapigwa na kila mtu. Miaka mitano iliyopita tulipata nini? The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate"
}