GET /api/v0.1/hansard/entries/729404/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 729404,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/729404/?format=api",
"text_counter": 343,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Tumefaidi nini?Tumenyimwa nini? Jamii ya Mkuria haina Waziri, balozi na hata kupata afisa mkuu anayesimamia kitengo cha polisi (OCPD) ni shida. Kuna “Ka-Mkuria” tu ambaye ni Kamishina huko Mombasa na anatwangwa twangwa na siasa na akina Joho. Ni huyo tu. Sisi ni Wakenya. Tuko kati ya yale makabila matano ambayo yameorodheshwa ambayo hawakuweko katika nafasi za uongozi wa Kenya hii. Mkuria, Mdorobo, Muogiekina na Mmaasai. Sisi ni watu au tuna mikia? Sioni pembe kwa kichwa changu. Mimi ni binadamu. Siku zilizobaki miezi kadhaa yatosha. Wewe Mhe. Rais Uhuru si kijana tena bali ni mzee. Ukishapitisha miaka 45 wewe ni mzee. Angalia kitabu chako na stakabadhi zako ulizoziweka. Panua utawala wako. Angazia kila sehemu ya nchi. Hutapata shida wengine wakinasanaswa, lakini usipolenga mawazo yako hivyo, basi hata Ulingo ni mkubwa. Twataka tuuone ujenzi wa nafasi ya meli katika ziwa Victoria. Meli zilikuwepo kabla Uhuru. Zilitapakaa, zikaharibika na hakuna aliyejali. Tunataka tuone usafiri huo na mipango ya kilimo bora. Huko kwetu kulikuwa na tobako. Tukaharibu misitu na sasa tumeanza kuona watu wanashikwa na kansa hapa na pale. Twakataa tobako. Kuna nafasi ya kilimo cha nafaka tofauti. Kuna mimea ya kutoa mafuta ijulikanayo kama soya beans . Tuletee viwanda. Huenda sisi hatuna nguvu kama wengine walio matajiri. Tutafutie marafiki waje huku ili tujiskie kwamba uchumi wa nchi ya Kenya na matunda ya Uhuru yanaonekana. Usalama ni jambo ambalo Rais aliguzia kidogo. Ingawa ni haki tuwe na wanajeshi kule Somalia, tunapopata shida hapa Pokot, ya nini kurundika maaskari kule? Tunajitafutia shida na Al-Shabaab. Limbukeni hilo. Tuliambiwa kuwa askari mmoja anahudumia watu 390 na wanatosha kulingana na kiwango cha Umoja wa Mataifa. Lakini je, maaskari hao wako wapi, wanalinda nani na wanafanya kazi gani? Wanafaa warudi watumikie wananchi."
}