GET /api/v0.1/hansard/entries/729406/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 729406,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/729406/?format=api",
    "text_counter": 345,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Hatujui kwa nini makabila yapigane. Kwa nini Mturkana apigane na Mpokot? Kwa nini Mmaasai apigane na Mkuria? Ni kwa sababu rasilimali bado haijaenezwa vilivyo. Watu wanapigania maji na juzi tuliambiwa kwamba maji yanayoweza kunywewa na Wakenya kwa miaka 75 yamepatikana Turkana. Mbona watu wanapigania maji? Mitambo ipelekwe na maji yatekwe ili Waturkana na Wapokot wapate maji ya kutosha na ng’ombe, mbuzi, kondoo na ngamia wanawiri. Hamna mtu atakayeenda kupiga mwingine kwa kukosa lishe ya mifugo. Sasa, wanajamii wameanza kuwapiga Wazungu waliobaki kwa sababu wanafikiri wamechukua mito yao. Bw. Naibu wa Spika, ningependa kuendelea lakini asante."
}