GET /api/v0.1/hansard/entries/729498/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 729498,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/729498/?format=api",
    "text_counter": 39,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Mwadeghu",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 98,
        "legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
        "slug": "thomas-mwadeghu"
    },
    "content": "Asante Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii ili nitoe sauti yangu kwa haya machache ambayo yamejiri hapa katika ukumbi huu. Nakubaliana na wenzangu kuwa ni muhimu Wabunge wasome na waelewe hizi sheria ambazo tunataka kuzipitisha kwa sababu nyingi zao, wasipozisoma, zitawaadhiri hao waliopo hapa na wengine wanaokuja. Mara nyingi, huwa tunakutwa na hizi sheria tukiwa tumetoka Bungeni na sisi wenyewe hatujazisoma. Hata hivyo, si jambo la kuchukulia kiholela kuwa tunaleta sheria Bungeni za kuangalia uchaguzi utakuwa wa aina gani halafu Wabunge wenyewe wawe hawajazisoma, hawajazielewa wala hawazitambui. Wanaenda kuleta zogo huko mtaani baada ya kutoka hapa. Vile nilivyosema narudia leo kuwa asilimia themanini ya Wabunge hawatarudi kulingana na tarakimu zilizopo. Kwa hivyo, wengine ambao mko hapa na hamtaki kusoma sheria, hamtarudi hapa Bungeni. La mwisho, sikubaliani na mwenzangu Mhe. Duale akisema kuwa Gavana wa CBK, kwa sababu ni Mkatoliki, haweki hela kwa benki na hana akaunti. Ile ni imani yake ya kutoa kile chote amepewa kuwapatia wale ambao hawana. Hata wewe unaweza amua kuishi maisha hayo. Hiyo haimanishi kuwa huwezi kuendesha kazi ya kuwa gavana wa benki. Hayo hayakuweko wakati aliomba kazi. Aliomba kazi, mkamwajiri mkijua ni Mkatoliki na mkijua anashikilia imani yake. Haamini kuweka fedha na kujitajirisha. Kwa hivyo, naomba Mhe. Duale ayaondoe haya matamshi kuwa huyu bwana hawezi kazi kwa sababu hana akaunti kwa benki. Sikubaliani naye kabisa. Sitakubaliana naye sasa. Hata nikiwa Gavana wa Taita Taveta, sitakubaliana na msimamo kama huo. Mungu awabariki."
}