GET /api/v0.1/hansard/entries/729629/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 729629,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/729629/?format=api",
    "text_counter": 170,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Mwanyoha",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 2308,
        "legal_name": "Hassan Mohamed Mwanyoha",
        "slug": "hassan-mohamed-mwanyoha"
    },
    "content": "Masuala ya visodo ni muhimu. Naona ni kama elimu ya msingi imeachiwa serikali za kaunti, lakini wameshindwa kuishughulikia. Kwa hivyo, tunataka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ihakikishe kwamba inatia mkono wake kikamilifu katika shughuli hizi ili watoto wapate elimu ya msingi itakayowafaa siku za baadaye. Hili ni jambo ambalo limeshughulikiwa na Hazina ya Kitaifa ya Maendeleo ya Maeneo Bunge (NG-CDF). Sipigii debe NG-CDF kwa sababu mimi ni mhusika, lakini ukiangalia shughuli ambazo NG-CDF imefanya, ziko juu zaidi kuliko zile zilizofanywa na serikali za kaunti. Kwa hivyo, masuala ya NG-CDF yaingizwe ndani, ili waweze kuhakikisha wanashirikiana ili elimu ya msingi iboreshwe zaidi."
}