GET /api/v0.1/hansard/entries/730225/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 730225,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/730225/?format=api",
"text_counter": 221,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "kipindi hiki cha miaka tano. Hata hivyo, Ni hotuba ambayo ilididimisha matumaini ya Wakenya wote. Wakati huu tunazungumzia juu ya ujenzi wa reli the Standard Gauge Railway (SGR). Tunameambiwa kuwa reli hii inatoka Mombasa hadi Nairobi na kisha itafika Naivasha na baadaye itafika Bungoma. Hata hivyo, mhe. Rais hakusema ukweli katika hotuba yake kuhusu gharama ya ujenzi huu wa reli hi ya SGR. Reli hii inajengwa kwa gharama ya juu sana. Ujenzi wake utakuwa maradufu bei iliyokusudio hapo awali. Mwanzo wake tuliambiwa itagharimu Kshs390 billioni. Kuna pesa nyingi ambazo zimekwenda katika mifuko ya watu binafsi. Ni hatua gani mhe. Rais amewachukulia watu hao ambao wamejitajirisha na ujenzi wa reli hii? Aya ya kumi ya hotuba yake inasema ya kwamba demokrasia yetu imenawiri sana. Ukweili ni kwamba demokrasia katika nchi hii imezoroteka. Mhe. Rais mstaafu Bw. Mwai Kibaki alituambia yote yawezekana katika demokrasia. Tuliona mwananchi akiweza kupiga kelele barabarani, kuhubiri madukani, kufanya biashara na kuwa na maandamano ya kila aina. Haya yote yalifanyika katika uongozi wake na hakuweza kukasirika. Hivi sasa ni kama tumerudi katika enzi ya miaka ya 1992 wakati wanasiasa wetu washupavu walikimbilia nchi za kigeni kwa usalama wao. Kwa mfano, Sen. (Prof.) Anyang’-Nyong’o na wengine walihamia nchi zingine kwa sababu ya kuogopa kushikwa na polisi na kutiwa mbaroni. Mhe. Rais alisema katika demokrasia yetu kila mtu ana uhuru wa kufanya lolote analolitaka. Lakini jambo la kushangaza ni kuwa wakati wanasiasa wanapozunguka hapa na pale, wakati wa uongozi huu wa Jubilee, tunaona hali ni tofauti kabisa. Mimi nikiwa mmoja wa wale watu waliokuwa wakizunguka huko Pwani tukienda kusalimia ndugu zetu wa Mpeketoni katika Kaunti ya Lamu tulipigwa mawe na tukarushiwa maembe na magari yety yakaharibika vibaya sana. Ilibidi tukimbilie usalama wetu. Mkutano haukufanyika siku hiyo. Je, hii ndio demokrasia mhe. Rais alizungumzia katika hotuba yake katika Bunge la Kitaifa? Tuliona demokrasia imepotea, hasa katika upande wa Kinango wakati wanasiasa wengine huko Pwani walikuwa katika harakati zao za kukutana na wafuasi wao. Wakati helikopta ilitaka kutua chini, Gavana Hassan Ali Joho namwenzake Amason Jeffah Kingi, Gavana wa Kilifi,hawakukubaliwa kushuka chini ambapo mkutano uliandaliwa. Mambo yaliyotendeka huko Lamu na kwingineko ni kinyume kabisa ya hotuba ya mhe. Rais katika Bunge la Kitaifa hapo tarehe 15-03-2017. Kumekuwa na changamoto tofauti tofauti. Katiba yetu ya Kenya inasema ya kwamba mkenya ana haki ya kufanya biashara na kujiendeleza kimaisha na huwezi kumzuia mkenya kupata mapato yake katika utendakazi wake ama kujikimu kimaisha. Hata hivyo, katika Serikali ya Jubilee, wafanyabiashara wengi ambao hawawezi kuunga mkono Serikali akiwemo Hassan Ali Joho wanafuatwa na maafisa wa Kenya RevenueAuthority (KRA) . Simsemi Joho kama gavana bali kama mfanyabiashara. Juzi aliandikiwa barua na KRA na huo ni ukiukaji wa Katiba ambayo Rais mwenyewe katika hotuba yake alisisitiza. Alisema kwamba Katiba ndio inafuatiliwa na sheria zake ndio muhimu katika nchi yetu. Vile vile, Rais katika hotuba yake alisema kuwa kila mtu ana uhuru katika Kenya. Hata hivyo, akiwa pwani hasa alipokuwa amekwenda kufungua miradi fulani, Rais The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate"
}