GET /api/v0.1/hansard/entries/730227/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 730227,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/730227/?format=api",
"text_counter": 223,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "alitumia matamshi ambayo yalileta taharuki. Hivi sasa watu wa pwani hawajui kwamba kutatendeka nini tena. Alisema kuwa yeye kama Rais wa Jamhuri ya Kenya atamnyorosha. Alitumia msemo huo kwa mwanasiasa. Huo ni ukiukaji wa hotuba aliyotoa ndani ya Bunge. Kuambia mkenya mwingine kuwa utamnyorosha ni kumtishia maisha. Ukisema hivyo kisha kutokee kitu fulani, watu watajua kuwa vile ulivyosema na nia yako ilikuwa kumnyorosha mtu yule. Sasa hivi, maafisa wengi wanaenda kila mahali. Kuna maafisa wa KRA wanaofanya uchunguzi na kisha tunaambiwa maafisa wa Kenya National ExaminationCouncil (KNEC) watachunguza vyeti. Kumekuwa na mahojiano mengi na sasa hata hawezi kufanya kazi yake ya ugavana kisawasawa. Sisi tunasema kuwa viungo tofauti tofauti ambavyo viko chini ya Katiba vinafanya kazi yake vikiwa huru. Haviko chini kuonyeshwa njia na Ofisi ya Rais ama Mawaziri wake. Vile vile katika hotuba yake, Rais alisema ya kwamba tulichukua hatua ya kihistoria mwaka 2011. Hiyo ilikuwa hatua ya kupeleka vijana wetu wa jeshi kuingia Somalia. Kulingana na Rais, tulichukua hatua hiyo kwa sababu nchi yetu ilikuwa katika hali ya hatari. Tulipeleka vijana wetu huko kuanzia mwaka 2011 hadi sasa mwaka 2017. Hususan hiyo ni miaka saba tukiwa ndani ya Somalia. Je, tumetengeneza makaburi mangapi ya vijana wetu wanaorudishwa nyumbani wakiwa ndani ya maplastiki meusi? Je, ni wanawake wangapi walioachwa wajane katika nchi yetu ya Kenya? Kuna lazima gani ya sisi kuendelea kuwa Somalia zaidi ya miaka saba? Je, tunafikiria kuwa hatutengenezi chuki ikiwa majeshi yetu yako ndani ya Somalia? Wimbo wetu wa Taifa unazungumzia nchi tunayoipenda na kuwa tutazidi kuilinda. Tutailinda nchi yetu tukiwa ndani wala si nje. Tunamtaka Rais atuambie ni lini majeshi yetu yataanza kurudi nyumbani. Si jambo jema kuendelea kutengeneza makaburi kwa sababu watoto wetu wako katika nchi ya wenyewe. Kama Al-Shabaab wako huko na wanataka kuendelea kumalizana, waache waendelee na maisha yao. Juzi wametengeneza serikali yao na wako na rais, mawaziri na wakuu wa majeshi na polisi. Majeshi yao yanafanya nini ikiwa majeshi yetu yako huko? Ni kitu gani kinaweka majeshi yetu katika nchi ya Somalia? Hilo ni swali ambalo Wakenya wanataka kujua. Rais vile vile katika hotuba yake alitaja kwamba kuna miradi tofauti tofauti ambayo alikuwa amekwenda kufungua ikiwemo ile ya Kilifi. Katika Kaunti ya Kilifi kuna kituo cha utamaduni. Rais ni mtu mkubwa sana kwenda kufungua miradi midogo midogo ambayo hata mingine si ya Serikali yake. Je, huo ni ungwana? Alienda kufungua kituo cha utamaduni kule Chonyi kilichojengwa na Kaunti ya Kilifi. Gavana alitaka kwenda kufungua lakini akakatazwa kuwa Rais ndiye angefungua. Mwishowe ilikuwa ushindani na hatimaye ikabainika wazi kuwa kituo hicho cha utamaduni kilitengenezwa na Kaunti ya Kilifi. Hiyo ndio ilimfanya Rais kutoenda kukifungua. Vile vile Rais alitaka kwenda kufungua feri ambayo imekuwa kwa miaka 40. Ni feri kongwe ambayo haifai na inasaki katikati ya bahari raia wakiwa ndani. Je, hiyo ni haki? Ikiwa Rais anataka kufungua mradi, anafaa kufungua mradi wa kisawasawa ambao watu wa pwani watafurahia. Anafaa kufungua mradi wa kisawasawa ambao watu wa Kilifi wanajua umefanywa na Serikali ya kitaifa."
}