GET /api/v0.1/hansard/entries/731985/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 731985,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/731985/?format=api",
"text_counter": 478,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Wanyama",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1076,
"legal_name": "Janet Nangabo Wanyama",
"slug": "janet-nangabo-wanyama"
},
"content": "huwa tunapinga sana katika nchi yetu kwa sababu yanatuletea madhara. Unapata mtu amehitimu lakini ukimpa kazi afanye, hafanyi kwa njia sawa kwa sababu hakutumia njia mwafaka ya kuhakikisha kwamba anafika penye amefika. Ninataka kuunga mkono Mhe. Agoi kwa kuleta huu Mswada katika Bunge hili, wa kuhakikisha kwamba tuko na jopo kazi la kuhakikisha kwamba kuna usawa. Iwapo kutakuwa na matatizo ama iwapo tutakuwa na mambo yale yasioeleweka katika nafasi ya mtu kuhitimu ama ya kupewa cheti chake – tunafahamu yaliyompata Mhe. Joho - hilo jopo kazi litasaidia wananchi ambao hawana nafasi ya kujitetea. Tena, ni aibu kubwa sana kwa sababu ikifika uchaguzi, jopo kazi la uchaguzi na mipaka linaingilia kati na kusema kwamba wanatafuta hiki na kile. Jambo kama hili linaelekea kutumua vibaya ushuru wa wananchi katika nchi yetu. Hatuna barabara na maji sehemu zingine ilhali tunatumia ushuru vibaya. Badala ya matumizi mabaya ya hizi pesa, ni heri zipelekwe kule mashinani zilete maendeleo katika nchi yetu. Namshukuru Mhe. Agoi kwa kuleta Mswada huu ili sisi kama viongozi katika Bunge hili tuuchangie na kuona kwamba sekta ya elimu katika nchi yetu imeendelea mbele na inaleta usawa. Bila elimu, watoto wetu na vizazi vijavyo havitapata nafasi ya kuwa viongozi. Usipokuwa na elimu, watu wanasema kuwa Serikali haijapeana kazi ya kutosha. Lakini mtoto akihitimu, akipata cheti chake, licha ya kwenda katika chuo kikuu, anaweza kwenda katika chuo cha kiufundi. Hiyo inaendelea kuongeza maarifa zaidi na inawapatia nafasi ya kupata kazi katika sekta mbalimbali katika nchi yetu. Ahsante sana. Naunga mkono Mswada huu."
}