GET /api/v0.1/hansard/entries/732116/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 732116,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/732116/?format=api",
"text_counter": 74,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Korere",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13134,
"legal_name": "Sara Paulata Korere",
"slug": "sara-paulata-korere"
},
"content": "Ninashukuru Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii kuchangia Hotuba ya Mtukufu Rais kwa taifa tukufu la Kenya. Waswahili husema “aliye na macho haambiwi tazama”. Ndiposa nasimama mbele ya Bunge hili nikishangaa sana vile wapinzani wetu wanaongea. Kaka aliyesema mbele yangu amenishangaza kwa sababu anapotoka yeye, barabara ya lami ilifika baada ya Serikali ya Jubilee kuchaguliwa. Rais alizungumzia kuhusu vita dhidi ya uraibu wa madawa ya kulevya katika nchi tukufu ya Kenya. Hakuna Serikali nyingine ambayo nimeona ikipigana na janga hili la madawa ya kulevya na uraibu wake jinsi Serikali ya Jubilee ilivyopigana nayo. Vizazi vyetu haswa vijana wanaangamia kwa sababu ya madawa ya kulevya. Cha kushangaza, waraibu wakuu na wenye biashara kuu za madawa za kulevya ni watu ambao wana sifa kocho kocho katika nchi hii. Wamesikika na wameshikilia nyadhifa kubwa kubwa katika nchi hii na ni watu ambao wana nia ya kugombea kiti cha Urais katika nchi hii. Ndio maana ningependa kumwambia Rais wangu apigane na vita vya madawa ya kulevya, aokoe vizazi vyetu na vijana wa nchi hii."
}