GET /api/v0.1/hansard/entries/732117/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 732117,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/732117/?format=api",
"text_counter": 75,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Korere",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13134,
"legal_name": "Sara Paulata Korere",
"slug": "sara-paulata-korere"
},
"content": "Suala lingine nyeti ambalo Rais alizungumzia katika Bunge hili ni usalama. Yale ambayo tumeona yakifanyika haswa katika baadhi ya kaunti kama vile Laikipia ninakotoka, Kaunti ya Baringo, hawa ni majambazi ambao ni Wakenya na wanaangamiza wakenya wengine. Hii ndio maana ninataka kumpa heko hata kwa kutuma jeshi kwenda kudhibiti usalama. Rais anapozungumza kuhusu kupatia kazi vijana, tunaelewa biashara ambayo sisi Wanalaikipia tunafanya. Biashara ambayo iko Laikipia ni biashara ya utalii. Biashara ya utalii katika Laikipia inaenda kuangamia kwa sababu ya ujambazi na jinsi tulivyoona mahali pa utalii pakiharibiwa. Baadhi ya mambo ambayo yameharibu usalama na kuchangia sekta ya utalii kufa Laikipia ni siasa duni ambayo imechangiwa sana na wapinzani wetu. Hii ndio maana ninasema aliye na macho haambiwi tazama. Iwapo tutaua sekta ya utalii nchini, kazi kwa vijana itatoka wapi? Wale wanachangia katika kuua sekta ya utalii nchini wanatarajia kuchaguliwa kesho. Hawa ndio tunawaita mahasidi wasio na mbele wala nyuma. Tukitazama mambo ya ugaidi nchini na mipaka ya Kenya, ni sharti tupigane nayo. Jumamosi iliyopita tuliona Rais akitembelea vikosi vyetu vya jeshi kule Somalia. Ningeomba The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}