GET /api/v0.1/hansard/entries/732124/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 732124,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/732124/?format=api",
    "text_counter": 82,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Wanyama",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 1076,
        "legal_name": "Janet Nangabo Wanyama",
        "slug": "janet-nangabo-wanyama"
    },
    "content": "Asante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii nichangie Hotuba ya Mhe. Rais. Kwanza, ningependa kumshukuru Mhe. Rais kwa ajili ya kazi ambayo amefanya katika nchi yetu ya Kenya, haswa kuleta umoja kwa Wakenya. Mhe. Rais aliongea kuhusu mambo ya elimu katika nchi yetu ya Kenya. Mwenzangu mmoja amesema kwamba watoto wetu wakihitimu, wengine hawapati kazi. Katika darasa la nane na kidato cha nne, watoto wanafanya mitihani bila kulipa kitu chochote. Kuna watoto wengine wakifika katika kidato cha nne huwa hawahitimu kujiunga na vyuo vikuu. Mhe. Rais aliongea vizuri sana kuhusu jambo hili. Tuna macho na tumeona kuwa tuna vyuo vya ufundi, mahali tunapeleka watoto wetu ambao hawajahitimu kwenda chuo kikuu. Hiyo haimanishi kwamba watoto wetu wako na ujuzi wa kutosha kufanya kazi katika nchi yetu ya Kenya, haswa katika sekta mbalimbali. Jambo la pili, Rais alisema kwamba mnaweza kuona upande wa usalama katika nchi yetu ya Kenya. Tulikuja katika Bunge hili, tukapata kwamba wanajeshi wetu walikuwa wameenda kule Somalia kwa sababu ya kuleta usalama katika nchi ya Kenya na nchi jirani ya Somalia. Hawakutumwa waende kuwauwa, bali walikuwa wameshika doria kuhakikisha kwamba nchi jirani iko na usalama na sisi pia tuna usalama. Katika Hotuba yake, Mhe. Rais aliongezea kuwa wale waliopoteza maisha yao wakipambana na wahalifu, familia zao zilikuwa zinapewa fedha za kuendelea na maisha. Pia, Mhe. Rais aliongea kuhusu barabara. Ni hakika barabara zimetengenezwa. Ndugu zangu kutoka Wajir ama kaskazini mashariki ya Kenya walisema kwamba wamepata maendeleo kwa muda wa miaka mitano. Huu ni mwaka wa tano. Hapo awali kulikuwa na viongozi katika The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}