GET /api/v0.1/hansard/entries/732125/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 732125,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/732125/?format=api",
    "text_counter": 83,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Wanyama",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 1076,
        "legal_name": "Janet Nangabo Wanyama",
        "slug": "janet-nangabo-wanyama"
    },
    "content": "Bunge hili na Rais lakini hawakujaribu kufikia kiwango kile Mhe. Rais amefikia kwa miaka mitano. Heko kwa Mhe. Uhuru Muigai Kenyatta. Mhe. Rais hakukosea kuzungumza kuhusu changamoto. Changamoto zinatokana na ufisadi katika nchi yetu. Tukumbuke kwamba si Rais analeta ufisadi bali baadhi ya wanaoshikilia ofisi kuu. Katika Bunge hili, mtu akishikwa kuwa mfisadi, watu wanaibadilisha inakuwa ni ukabila. Wanasema huyu ni wangu ameshikwa, huyu ni wangu anaonewa. Rais akisema mshukiwa huyo anatakikana afanywe hivi, mtu mwingine anasema hapana. Huyu anatoka upande wangu, yaani upande wa Upinzani au wa Serikali. Mfisadi ni mfisadi, hata awe ndani ya kanisa ama ndani ya nyumba yako. Ninaunga Rais mkono. Inafaa sisi viongozi katika nchi hii ya Kenya tujue kwamba tuko na ufisadi na lazima tupigane nao. Kuna pesa ya wazee na ninafurahi kwa sababu inaboresha jamii ya Kenya. Pesa hizo hazikuwa zinafikia wazee wa enzi zile, lakini sasa unaweza kuona kwamba wazee wanafurahia kwa sababu hizi pesa zinawasaidia. Kuna watoto kutoka jamii maskini ambao hupata hizi fedha. Licha ya kuwa na hazina ya maendeleo katika maeneo ya Bunge, Rais pia amejitolea kutoa zake mwenyewe binafsi kufikia jamii isiyojiweza katika Kenya. Ninamuunga mkono Rais kwa kazi mzuri. Tumpatie tena miaka mitano. Heko kwa Rais."
}