GET /api/v0.1/hansard/entries/732127/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 732127,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/732127/?format=api",
"text_counter": 85,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Gathogo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 2715,
"legal_name": "Esther Nyambura Gathogo",
"slug": "esther-nyambura-gathogo"
},
"content": "Asante sana Mhe Spika wa Muda kwa kunipa hii nafasi niweze kuchangia Hotuba ya Mhe Rais wa Jamhuri ya Kenya, Uhuru Muigai Kenyatta. Mengi yamesemwa na wale ambao wameongea mbele yangu. Mhe Rais hakutaja mambo yote ameyatenda. Watu wote wanasema amefanya miaka tano. Ninashangaa vile tunahesabu miaka kwa sababu tulimaliza miaka nne mwezi wa tatu ilhali ile kazi ambayo tunaongea juu yake ni kama ya miaka kumi. Tumeshukuru vile Mhe Rais amejaribu hata kuwaunganisha Wakenya. Kuwaunganisha Wakenya ni jambo moja muhimu kuliko kujenga barabara, reli ama madarasa. Mhe. Naibu Spika wa Muda, sisi kinamama tulikuwa tumesahaulika. Wakati Serikali ya Jubilee ilipochukua hatamu ya uongozi, tulitambulika na kupatiwa viti kadhaa. Hakuna ufisadi kinamama wanapoongoza. Tukiangalia katika maeneo Bunge yetu, tunaona watu wengi wanasema kwamba Rais hajafanya kazi. Tukiwa katika Bunge la Kitaifa, wapinzani wetu katika maeneo Bunge wanasema hakuna kazi yoyote ambayo tumefanya ilhali sisi tunajua kwamba tumefanya kazi. Kama kila mtu amefanya kazi katika eneo Bunge lake, sielewi ni kwa nini tunasema Rais hajafanya kazi. Pesa ambazo tumetumia kutekeleza miradi katika maeneo Bunge zimetoka kwa Serikali. Kama umejenga madarasa katika eneo Bunge lako, umesaidia. Umetoa pesa kujenga madarasa hayo na kufanya mambo mengine mengi. Basi kwa nini tuseme kwamba Serikali ya Uhuru Muigai Kenyatta haijafanya kazi? Hii ni kumanisha kwamba wewe unayesema hivyo hujafanya kazi katika eneo Bunge lako. Ninafuraha sana kwa sababu kinamama tulipoondolewa malipo ya huduma ya uzazi kwenya hospitali za umma, watoto wameongezeka kwenya eneo Bunge langu la Ruiru. Watu The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}