GET /api/v0.1/hansard/entries/732128/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 732128,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/732128/?format=api",
    "text_counter": 86,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Gathogo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 2715,
        "legal_name": "Esther Nyambura Gathogo",
        "slug": "esther-nyambura-gathogo"
    },
    "content": "wakiongezeka, kura pia zitaongezeka. Jana nilitembelea Hospitali ya Ruiru, ambako nilishuhudia madawa na vifaa vingi vya matibabu vikipelekwa pale. Hii ni kwa sababu Serikali inafanya kazi. Kwenye ghala la madawa niliona vifaa ambavyo hutumiwa kuwasaidia kinamama wakati wanapojifungua. Kwa hivo, yangu ni kusema kwamba Rais wa Jamhuri ya Kenya, Mhe. Uhuru Muigai Kenyatta, amefanya kazi kubwa katika kipindi cha miaka minne.Tunamuunga mkono kwa sababu yeye ni Rais wa kwanza kushikilia uongozi wa Serikali yenye viwango viwili – serikali za kaunti, ambazo ziko na magavana na Serikali ya kitaifa, ambayo ina Wabunge. Pia, ninampongeza kwa sababu ametuunganisha sisi sote; makabila yote katika nchi ya Kenya. Kwa hivyo, Mhe. Uhuru Muigai Kenyatta yuko sawa. Tunasema aendelee na kazi, kama Esther Gathogo kutoka eneo Bunge la Ruiru alivyosema “mama aendelee na kazi”. Ahsante, Mhe. Naibu Spika wa Muda."
}