GET /api/v0.1/hansard/entries/732215/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 732215,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/732215/?format=api",
"text_counter": 173,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Bedzimba",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1933,
"legal_name": "Rashid Juma Bedzimba",
"slug": "rashid-juma-bedzimba"
},
"content": "Ahsante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii kuchangia Hotuba ya Mhe. Rais. Kwa kweli, taifa nzima lilikuwa linatarajia mengi kutoka kwa kinywa cha Mhe. Rais kuliko hata yale ambayo aliyazungumza. Kwanza, Wakenya walikuwa wanataka yeye kama Amiri Jeshi Mkuu atueleze hali halisi ilioko nchini Somalia ambako vijana wetu wa kike na wa kiume katika sare rasmi wanapoteza maisha yao. Pia, tulikuwa tunatarajia atakuja kuzungumzia idadi ya wanajeshi waliopoteza maisha yao kule ni wangapi, na wale ambao wameachwa bila waume wao wanasaidiwa namna gani. Vile vile, tulikuwa tunatarajia atueleze ameelekea vipi na Wizara ya Mambo ya Nje kuhusu suala ambalo Wabunge wa Bunge la Somalia wakati fulani walipitisha, kuwa hawataki wanajeshi ya Kenya wawe kule. Kwa hivyo, tulitaka pia atueleze Wizara yake imekaa na wale Wabunge wa taifa la Somalia na atueleze sasa wamefikia mpango gani na wamekubali wanajeshi wetu wafanye nini. Bila hivyo, sisi tunafikiria kama Wakenya kwamba kulingana na vile Wabunge walikataa Jeshi la Kenya kuwa kule, wao ndio wanafanya mipango wanajeshi wetu wavamiwe katika makambi yao. Kwa hivyo, sisi tunategemea kwamba wanajeshi wetu wataendelea kupoteza maisha yao ikiwa Serikali haitakuwa na makini kufuatia suala hilo."
}