GET /api/v0.1/hansard/entries/732218/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 732218,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/732218/?format=api",
    "text_counter": 176,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Bedzimba",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 1933,
        "legal_name": "Rashid Juma Bedzimba",
        "slug": "rashid-juma-bedzimba"
    },
    "content": "Mhe. Naibu Spika wa Muda, tukizungumzia habari ya stima ambayo Mhe. Rais alizungumzia, sasa shule nyingi zinakatiwa stima, zinakuwa kwa giza. Anasema kwamba yeye ameweka stima lakini shule nyingi zimeshindwa kulipa gharama ya stima. Shule nyingi zimerudi gizani. Hapo hajafuatilizia kujua hali halisi ilivyo. Akizungumzia kuhusu suala la barabara, sisi kwetu Mombasa tunasema, hata kama watu wanaona ni uchungu, hakuna barabara hata kilomita moja ama mbili ambayo imejengwa na pesa ambazo tunalipa kama kodi. Barabara zinajengwa kule karibu zote ni zile ambazo tunapata misaada na mikopo kutoka Benki ya Dunia ama Uingereza. Sasa, hapo ndio anasema ametengeneza barabara lakini kwetu kaunti ya Mombasa hatuoni. Hata mimi wakati moja tulikaa na Mhe Rais na Naibu wake tukazungumzia barabara ya Mwakirunge. Hata mimi katika pesa zangu za NG-CDF nilitaka kuanza kutengeza nusunusu wakaniambia, “Usitengeneze. Tutatengeneza sisi kama Serikali kuu.” Hakuna kitu ambacho wamefanya. Kwa hivyo, sioni kama amezungumzia mambo ya maana sana. Kuhusu reli, alisema tarehe moja Juni twende tukapande reli tukuje. Reli ile ni kuukuu. Ile ni reli ambayo ni second-hand, sio ile wananchi walikuwa wanataka - ile ya kuenda mbio. Ile ni kama ya zamani tu imepakwa rangi."
}