GET /api/v0.1/hansard/entries/732476/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 732476,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/732476/?format=api",
"text_counter": 250,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Bady",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1612,
"legal_name": "Bady Twalib Bady",
"slug": "bady-twalib-bady"
},
"content": "mwenzangu Mhe. Waluke alivyozungumza hapa kuhusu Serikali. Alisema karibu miaka 26 iliyopita, hakukuwa na maji kwake na leo ameona maji ya mifereji kwake. Mimi ninatofautiana vikali kabisa kwa sababu katika kaunti yangu ya Mombasa na viunga vyake, leo tunalia hatuna maji miaka mingi baada ya kupata Uhuru. Watu wakiona maji ni kama wameona almasi. Ni juzi tu, Mhe. Rais alipokuwa Mombasa ndivyo Waziri wa maji, Bwana Eugene Wamalwa alisema anatambua jambo hili ni la kweli. Lakini watu wa Mombasa watakaa kwa miezi sita ili waende kukopa pesa ili waangalie vile watarekebisha. Miaka hii yote watu wamekua wakiteseka, tutasubiri tena miezi sita? Hili si jambo ambalo Serikali inafaa kuliweka kando. Maji ni uhai na ni lazima yaletwe kwa wananchi. Ukiangalia sehemu yangu ya Jomvu, utaona kila siku ninasema jambo hili Mikindani, Miritini na Jomvu Kuu. Ukitembea barabarani, mabomba yaliyoletwa na World Bank, yamekaa kando ya barabara badala ya kuchimbwa na kuwapa watu maji. Jambo hili ni la kusikitisha. Ukipita barabara ya kutoka Nairobi kupita Jomvu, utapata watu wamekaa na mitungi kutafuta maji barabarani. Utasikitika watu wako kwa hali mbaya. Sina haja ya kusema mambo ya maji zaidi ya vile nimesema."
}