GET /api/v0.1/hansard/entries/732477/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 732477,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/732477/?format=api",
"text_counter": 251,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Bady",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1612,
"legal_name": "Bady Twalib Bady",
"slug": "bady-twalib-bady"
},
"content": "Jambo lingine ni ugatuzi. Rais hajasema ukweli wa vile hali ilivyo. Huwezi kusema kwa Bunge kuwa unaamini ugatuzi halafu ukitoka nje ya Bunge, unazuia vyombo vinavyohusiana na mambo ya ugatuzi. Ninasema hivi nikimaanisha kile kitendo kilichotokea juzi kilichompata Gavana wa Mombasa, Mhe. Ali Hassan Joho kwa kuzuiwa kuhudhuria jambo ambalo kila mmoja anajua la Kaunti. Sisi tulipitisha Katiba na tunajua kuwa huduma za ferry ziko katika kaunti. Leo hii kusema kuwa unaamini ugatuzi na vile vile kuangalia kuwa viongozi ambao wako katika mambo ya kusimamia ugatuzi unawazuia, sidhani maneno haya ni ya kweli. Ni lazima tukisema tunakunywa maji, tusiwaonyeshe tunakunywa maji kumbe ni pombe. Tukisema tunakunywa maji, tunywe maji. Nitasema vile ndugu yangu Mhe. Shakeel Shabbir alivyosema. Rais hana shida, lakini wale wanaomzunguka ndio wanaompa mawaidha ambayo hayana maana ama hayaeleweki. Hivi sasa, tunavyozungumza tuna jukumu la kumuangalia Rais."
}