GET /api/v0.1/hansard/entries/733638/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 733638,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/733638/?format=api",
    "text_counter": 477,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Wanyama",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 1076,
        "legal_name": "Janet Nangabo Wanyama",
        "slug": "janet-nangabo-wanyama"
    },
    "content": "Ahsante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii angalau pia nichangie Mswada huu unaonuia kuzuia visa vya udanganyifu wa mitihani katika nchi yetu. Wenzangu wameongea kuhusu changamoto ambazo watoto wetu hupitia na pia, shida ambazo watangulizi wetu walizipitia hapo awali. Ni kweli vile wenzangu wamechangia. Kuna wengine wametoka katika maisha duni ama wamesoma kwa shule ambazo hazijajengwa vizuri katika maeneo yao. Mhe. Moroto amesema kwamba ukiona West Pokot mahali anatoka, wanafunzi walikuwa wakisomea chini ya miti. Sasa unaona katika maisha kama haya, wengine wakifika wakati wa kufanya mitihani yao halafu mwishowe isemekane kwamba mitihani imefutiliwa mbali, hiyo inaleta shida hata kwa jamii na wazazi wa watoto hao. Na siyo hiyo tu. Vile wenzangu wamesema, zile changamoto walimu wanapitia katika sehemu kama hizo za ukame na sehemu zinginezo ambazo hazina barabara ama hazina vifaa vya kutosha, ni nyingi. Shida hizo pia zinachangia katika mambo haya ya mitihani. Hapo awali, tulikuwa tunafanya mitihani ya darasa la saba. Kutoka darasa la saba, mtu akienda katika shule ya upili, wanafanya mtihani katika kidato cha pili. Ilikuwa inapatia mtu nafasi angalau kuona anaendelea mbele ama ako na nafasi ya kurudia hicho kidato. Hiyo ilikuwa inatupatia manufaa mazuri sana. Tukipata wale wamehitimu vizuri kutoka hapo, walielekea kidato cha nne na baadaye wakamalizia kidato cha sita kule mbele. Walikuwa wakiendelea vizuri sana. Lakini kulifika mahali tukawa na udanganyifu kwa sababu baadhi ya walimu na wazazi wale wanajitosheleza katika jamii wanatafuta njia za kuhonga walimu ama walimu wakuu, na hao walimu pia wanapata nafasi ya kutembea katika Mtihani House kuhakikisha kwamba watoto wao wanafanya vizuri katika shule zao, ama wanafanya vizuri kuhitimu katika madarasa waliokuwa wakifanya mitihani yao. Cha kushangaza ni kwamba, tulikuwa na mwenda zake Mheshimiwa katika Bunge hili, Mhe. Mutula. Mliona kwamba baada ya kukuwa waziri, alihakikisha kwamba amepatia mtoto wake shahada ya degree ilhali hakumaliza ile miaka inahitajika katika chuo kikuu. Sasa, unaona hao ni baadhi ya viongozi miongoni mwetu - wale walikuwa wakichangia mambo kama haya katika nchi yetu ya Kenya. Mtoto wa tajiri ama mtoto wa kiongozi anafaidika. Huyo kiongozi anapata nafasi ya kuhakikisha ya kwamba mtoto wake anapita mtihani bila hata kupitia masharti yale yanayotakikana katika sekta ya elimu katika nchi yetu. Na haya mambo ya ufisadi ndio The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}