GET /api/v0.1/hansard/entries/734448/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 734448,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/734448/?format=api",
"text_counter": 235,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Kombe",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 250,
"legal_name": "Harrison Garama Kombe",
"slug": "harrison-kombe"
},
"content": "ni wajibu wao kuhakikisha kwamba madaktari wanalipwa vyema na kuona kwamba kitengo hicho cha afya kinatiliwa maanani vilivyo. Wale ambao walipigania ugatuzi ni kidonda hivi sasa kwa Serikali ya Kitaifa na hawataki kukubali kwamba zote tulikosea. Ukweli usemwe na uongo ujitenge. Ningependa kuwaomba magavana wote wawajibike na kuhakikisha ya kwamba wanawalipa madaktari vyema. Si vyema kaunti zingine zilipe madaktari vizuri na wanaendelea na kazi na wengine wapo nyumbani kwa sababu ya kutolipwa vyema. Wale wanaolipa vizuri wanatoka Kenya ipi, na wale ambao hawalipi vizuri wanatoka Kenya ipi? Naunga mkono Hoja hii ya kuahirisha Bunge kwa muda mfupi kwa sababu nitakuwa na nafasi ya kumpokea Rais akiendeleza shughuli zake za maendeleo kwa upanuzi wa barabara kutoka Sabaki kuelekea Marafa, na kusambaza maji kwa wananchi. Hilo si jukumu la Serikali ya Kitaifa bali ni kazi ya kaunti. Serikali ya Kitaifa imejitolea mhanga kupitia Rais Uhuru Kenyatta kusambaza maji kwa wananchi. Ningependa kushukuru Serikali na kuwaomba wakaze mshipi na waendelee kusambazia wananchi maendeleo, na waache wanaopiga mdomo waendelee."
}