GET /api/v0.1/hansard/entries/734504/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 734504,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/734504/?format=api",
    "text_counter": 48,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Ikiwa jamii ya wa Talai ilifanyiwa dhuluma hizo wakati huo, basi ninajiunga nao kutaka haki ifanyike kwao. Si hao pekee, hata kaburi ya mama shupavu, Mekatilili wa Menza, haijulikani iko wapi. Tungetaka kujua alikozikwa. Mpaka leo jamii ya Miji Kenda hawana vyeti vya kumiliki mashamba yao. Kwa hivyo, hawawezi kukuza maeneo yao. Ni aibu kuona watu wananyakua mashamba ya wa Miji Kenda na kutengeneza viwanja vya kucheza golf na kadhalika. Si haki kuwa na uhasama kama huo. Wakati ni sasa wa kuona mashamba haya yamerudishiwa waakazi wa Pwani."
}