GET /api/v0.1/hansard/entries/736564/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 736564,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/736564/?format=api",
    "text_counter": 197,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Ngunjiri",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 1179,
        "legal_name": "Onesmas Kimani Ngunjiri",
        "slug": "onesmas-kimani-ngunjiri"
    },
    "content": "Mhe. Naibu Spika wa Muda, mimi sikutaja jina la mtu yeyote lakini kama mtu anajijue, ni haki yake ajijue. Hakuna haja ya kupongeza Serikali wakati ulikuwa upande huu, halafu baada ya mchujo uanze kuongea ubaya wa Serikali. Hivyo ni kukosa msimamo. Mambo yaliyo mbele yetu, tunahitaji kuyaangalia. Sisi ndio tunatengeneza sheria. Kama tunatengeneza sheria, tuwache kupiga kelele. Tuseme yale mambo ambayo tunaweza kutatua. Kama kuna shida ya jambo fulani, tuipendekeze, tuizungumzie na tuone mwelekeo ni upi. Lakini tukifanya mambo ambayo inatuhusu kama Wabunge ni lazima tujue kwamba sheria ya nchi hii haitengenezwi na Uhuru Muigai Kenyatta ama Raila. Ni sisi Wabunge! Kwa hivyo, tunahitaji ushirikiano mzuri wa kuangalia ni shida gani ili tuweze kujua ni jambo gani tunaweza kufanya kutatua jambo hili. Mambo haya yote yamefanyika tukiwa kwa hili Bunge. Na kama tulikuwa kwa hili Bunge---"
}