GET /api/v0.1/hansard/entries/736566/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 736566,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/736566/?format=api",
    "text_counter": 199,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Ngunjiri",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 1179,
        "legal_name": "Onesmas Kimani Ngunjiri",
        "slug": "onesmas-kimani-ngunjiri"
    },
    "content": "Bw. Naibu Spika wa Muda, haijalishi kama nitaongea mambo ya ukweli kama ninavyoyafahamu. Sisi tumechaguliwa hapa, tumekuja kisiasa. Na tulichaguana kisiasa. Kwa hivyo tukizungumza mambo yale yanayofaa na kuyasuluhisha kisiasa, nafikiri ni kweli. Tuzungumzie suluhisho tunaloweza kupata. Tunahitajika kukaa chini pamoja tuangalie ni jambo gani linalohitaji kurekebishwa kwenye huu Mswada. Tuzungumze ukweli. Kama kuna pahali ambapo kuna shida, ama kama Mswada huu ulipitishwa kwa njia mbaya, niko tayari kulizungumzia jambo hili ili tuone ukweli uko wapi. Sisemi hivyo kwa sababu ya siasa. Ninasema hivyo kwa sababu ya jukumu letu. Sisi tukiwa hapa, kama Wabunge, tunahitaji kuweka tofauti zetu kando na tukumbuke kwamba tulichaguliwa tutatue matatizo ya wananchi. Kama kuna jambo lolote lenye utata, tulijadili kwa uzuri. Tuwaweke Uhuru Muigai Kenyatta na Raila Odinga nje, tuzingatie jukumu letu la kutafuta suluhisho. Ni jukumu letu. Tumechaguliwa na wananchi kuwatetea. Tukianza kutoka nje ya upeo huo, mimi nitakataa. Ndiyo maana ninakataa. Ninawaomba wenzangu tukae tuliangalie jambo hili. Kama kuna shida ambayo inaonekana, nitakubali. Kama jambo lolote linahitaji majadiliano, tukubaliane ili tuweze kuisaidia nchi hii. Hakuna Upinzani na Serikali tukiwa kwenye Bunge The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}